MILAN DERBY: MAURO ICARD HAT TRICK YAIPA USHINDI INTER MILAN

Mshambuliaji wa wa Inter Milan Mauro Icard amefunga magoli 3 na kuweza kuipa ushindi timu yake ya Inter Milan dhidi ya Ac Milan kwenye mchezo wa ligi kuu ya Italia Serie A

Mchezo huo ambao ni ‘derby’ ulifanyika kwenye dimba la Guisseppe Meazza na matokeo ya mwisho yalikua ni Inter Milan ana magoli 3 dhidi ya magoli 2 ya Ac Milan..

Okwi airejesha Simba kileleni

TIMU ya Simba imefanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kusawazisha bao ‘jioni’ na kuambulia sare ya bao moja dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Simba waliuanza mchezo huo kwa kasi lakini jitihada zao ziliishia kwenye safu ya ulinzi ya Mtibwa huku wakipata pigo dakika za mwanzo baada ya straika John Bocco kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kupata maumivu.

Mtibwa walikuwa wa kwanza kupata bao lililowekwa nyavuni na Salmin Mbonde dakika 35 kutokana na mpira wa kona na kufanya Simba waende mapumziko wakiwa wanyonge.

Kocha Joseph Omog alilazimika kufanya mabadiliko mengine yasiyo ya kiufundi baada ya beki Salim Mbonde kuumia hivyo nafasi yake kuchukuliwa na Juuko Murshid.

Emmanuel Okwi aliipatia Simba bao la kusawazisha katika dakika za nyongeza kwa mpira wa adhabu ndogo uliotinga nyavuni moja kwa moja.

Matokeo hayo yameifanya Simba wafikishe pointi 12 sawa na Mtibwa, Yanga na Azam lakini wekundu hao wamekaa kileleni kwavile wana tofauti kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Mechi kati ya Prisons na Stand United imemalizika kwa sare ya bila kufungana kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

​TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 12.08.2017

Barcelona wanamgeukia sasa kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 25, kwa sababu Liverpool wamegoma kabisa kumuuza Philippe Coutinho, 25. (Independent)
Liverpool waliwaambia Barcelona wiki hii kuwa Philippe Coutinho, 25, bei yake ni pauni milioni 136.5. (Daily Record)
Barcelona bado wanamtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20, na watarejea na dau la pauni milioni 127. (AS)
Iwapo Barcelona watashindwa kumsajili Ousmane Dembele au Philippe Coutinho, wataamua kumfuatilia Ivan Perisic wa Inter Milan ambaye ananyatiwa na Manchester United. (Sport Italia)
Kiungo wa PSG Angel Di Maria, 29, huenda akachukuliwa na Barcelona kuziba pengo la Neymar. (Sport)
PSG wamempa Kylian Mbappe mshahara wa pauni milioni 16.4 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka mitano ili kumshawishi kuondoka Monaco. (L’Equipe)
Kylian Mbappe, 18, anataka kuhamia PSG lakini hakuna mkataba wowote uliofikiwa na uhamisho huo huenda ukafanyika msimu ujao. (ESPN)
Real Madrid wameacha kumfuatilia Kylian Mbappe na huenda wakaamua kumfuatilia kiungo mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26. (Don Balon)
Chelsea bado hawajarejea na dau lililoongezeka kumtaka kiungo wa Leicester Danny Drinkwater, 27, baada ya Leicester kukataa dau la pauni milioni 15. (Telegraph)
Tottenham wanazungumza na Ajax kutaka kumsajili beki wa kati Davinson Sanchez, 21, kwa pauni milioni 35. (Mirror)
Kiungo wa Real Madrid Isco, 25, amesaini mkataba mpya wa miaka minne ambao una kifungu cha kutengua uhamisho cha pauni milioni 637. (AS)
Real Madrid wameacha kuwafuatilia Thibault Courtois, 25, wa Chelsea na David De Gea, 26, wa Manchester United. (Don Balon)
Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Oliveirense, ya Ureno, Bruno Amorim, 19. (Noticias ao Minuto)
Manchester United hawatalipa zaidi ya pauni milioni 90 kumsajili Gareth Bale kutoka Real Madrid. (Dario Gol)
Tukutane baadaye katika BBC Ulimwengu wa Soka ambapo tutakutangazia mechi ya Chelsea v Burnley.
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumamosi njema.

PICHA 13: Samatta alivyotisha mechi zote 3 Pre-Season

Mbwana Samatta alianza safari yake ya ‘Pre Season’ Julai 8 kwa kuichezea Genk kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Lierse ya Ubelgiji

Licha ya kuingia akitokea benchi, nahodha huyo wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ alionyesha kiwango bora akiwasumbua sana walinzi Lierse

Dakika ya 84 Genk ikiwa inaongoza kwa bao moja, Samatta aliifungia timu hiyo bao la pili na kufanya iibuke na ushindi wa mabao 2-0

Baada ya mchezo huo Genk ikapumzika kwa siku tatu pekee kabla kuvaana na Willem II kutoka nchini Uholanzi, Julai 12.

Genk iliyopania kutisha msimu huu iliibamiza Willem mabao 4-0

‘Vurugu’ za Samatta ziliendelea kama kawaida

Mwisho wa siku akaifungia bao moja maridadi katika ushindi huo mnono

Hamu ya mashabiki wa Genk ilikuwa ni kuiona timu yao ikiibuka na ushindi katika mchezo wa kirafiki uliofuata dhidi ya vigogo Ajax.

Nyota huyo hakuacha kuwaonyesha kazi walinzi wa Ajax

Kuna wakati iliwalazimu kufanya madhambi ili kumpunguza kasi nyota huyo ambaye kipaji chake kilianza kuonekana kwenye timu ya mtaani kwao Mbagala jijini Dar es Salaam iitwayo Kimbangulile FC

Rafu hizo hazikumzuia Samatta kuendelea na ‘yake’

 

Kuna wakati mabeki wa Ajax walilazimika kumkaba wawili kwa pamoja

Lakini bado mtoto huyo wa afisa mstaafu wa jeshi la Polisi alifanikiwa kuwaacha solemba

Samatta aliifungia Genk bao moja katika sare ya mabao matatu dhidi ya Ajax

Baada ya kufunga katika mechi zote tatu za mwanzo za maandalizi ya msimu mpya wa ligi, Samatta anatarajiwa kushuka tena dimbani kesho timu yake ikipambana na Bocholt ya Ubelgiji kabla ya kumalizia kwa kuvaana na Everton Julai 22.

Up ↑