TAIFA STARS YAIKABILI MOROCCO UGENINI KESHO

Taifa Stars inatupa karata yake ya
pili ugenini kwenye mechi za
mchujo za Kombe la Dunia kwa
kesho (Juni 8 mwaka huu) kuikabili
Morocco (Lions of the Atlas)
kwenye Uwanja wa Grand Stade
hapa Marrakech, Morocco.
Ilipoteza ya kwanza ugenini dhidi
ya Ivory Coast mwaka jana, na
kushinda mbili mfululizo
nyumbani dhidi ya Gambia na
Morocco.
Mechi hiyo itakayochezwa kuanzia
saa 3 usiku kwa saa za Morocco ni
ya pili kwa Stars katika uwanja
huo ambapo mwaka juzi ilifungwa
mabao 3-1.
Washabiki wa Morocco
wanaonekana kuikatia tama timu
yao yenye pointi mbili tu nyuma ya
Ivory Coast inayoongoza kundi hilo
la C ikiwa na pointi saba
ikifuatiwa na Tanzania yenye sita.
Huo ni mtazamo wa washabiki,
lakini kwa upande wa timu
inaonekana imepania kujichomoa
katika nafasi za chini.
Kwa upande wa Kocha wa Stars,
Kim Poulsen amesema timu yake
imepania mechi hiyo, lengo likiwa
ni kuona inapata matokeo mazuri
baada ya dakika 90 za mechi hiyo
itakayokuwa chini ya refa Daniel
Frazier Bennett wa Afrika Kusini.
Amesema timu yake itacheza kwa
umakini na uangalifu kwa vile
wanajua wapinzani wao
wakicheza mbele ya washabiki wao
watakuwa katika shinikizo za
kushinda, jambo ambalo
wamejiandaa kukabiliana nalo.
Kwa upande wa maandalizi, Kim
amesema Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) na
wadhamini wa timu hiyo
Kilimanjaro Premium Lager
wameiandaa vizuri kwani iko
kambini kwa wiki tatu sasa na
kupata mechi ya kirafiki dhidi ya
Sudan iliyochezwa wiki iliyopita
nchini Ethiopia.
Stars iliifunga Morocco mabao 3-1
zilipokutana Machi 24 mwaka huu
jijini Dar es Salaa. Lakini
zilipokutana hapa Marrakech mara
ya mwisho mwaka 2011, Morocco
iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Kim amesisitiza kuwa kikosi chake
kimepania kufanya vizuri katika
michuano hii ya mchujo ya Kombe
la Dunia, ha hiyo inathibitishwa na
matokeo ya timu kadri
inavyoendelea kucheza mechi za
mashindano.
“Moja ya mipango yetu katika
mechi hizi za Kombe la Dunia ni
kushinda nyumbani, hilo hadi sasa
tumelifanya kwa asilimia 100.
Lakini ili tukae vizuri zaidi
tumekuja hapa Morocco kwa lengo
la kupata matokeo mazuri, ingawa
tunajua mechi itakuwa ngumi,”
amesema kocha huyo raia wa
Denmark.
Kwa hapa Marrakech mechi hiyo
imekuwa haizungumzwi mara kwa
mara, na kubwa ni kuwa
Wamorocco wengi wanaamini
kuwa timu yao ambayo hadi sasa
ina pointi mbili haina nafasi ya
kusonga mbele katika hatua
inayofuata ya michuano hiyo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF)
Marrakech, Morocco

image

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑