UJUMBE KUTOKA KWA TEMBA:’WASANII WANAOTUMIA DAWA ZA KULEVYA NI MACHIZI’

ImageMSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Aman Temba ‘Mheshimiwa Temba’ aweka wazi kuwa baadhi ya wasanii wanaotumia dawa za kulevya wanakosa akili na matokeo yake kuwa machizi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Temba aliweka wazi kuwa baadhi ya wasanii wanaotumia dawa hizo akili zao zinakuwa haziko sawa na kuonekana wa ajabu hata kwa jamii inayowazunguka.

Alisema wanaotumia hizo dawa utawagundua kutokana na matendo yao wanayoyafanya kuonekana kama wamerukwa na akili hata kama wanajificha.

“Mimi ningekuwa natumia dawa za kulevya ungenigundua tu kwani hata usingeweza kuongea na mimi wala kunifanyia mahojiano yoyote kwa njia ya simu, kwani wengi wao wanaotumia dawa hizo wanakosa ustaarabu kabisa” alisema Temba.

Aliongezea kuwa hawezi kutumia dawa hizo kwani bado anahitaji heshima na kujua malengo yake, hivyo hata hao wanaoacha kutumia dawa hizo ni bora wakatambua ni sababu zipi zilizowapelekea kujiingiza katika matumiz hayo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑