MWAKYEMBE AELEZEA JINSI MASOGANGE ALIVYOPITISHA DAWA ZA KULEVYA UWANJA WA NDEGE

image

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison
Mwakyembe jana ameanika majina
ya watu saba waliohusika kupitisha
mabegi tisa yaliyokuwa na kilo 180
za dawa za kulevya zenye thamani
ya Sh8 bilioni, Julai 5 mwaka huu
katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),
wakiwamo maofisa usalama wanne
wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA) na polisi mmoja.
Alisema mizigo ikishaondoka
mikononi mwa abiria hukaguliwa
tena kwa kutumia mbwa wa Idara
ya Usalama wa Taifa, lakini siku ya
tukio hilo mbwa hao walichelewa
na walitumika baada ya mizigo
kuingizwa kwenye masanduku ya
chuma.
“Kwa abiria watatu kuwa na mabegi
makubwa tisa yanayofanana si kitu
cha kawaida kukwepa jicho la
maofisa wa ushuru wa forodha na
vyombo vya usalama, sijui walikuwa
wapi siku hiyo?” alihoji
Mwakyembe.
Juzi waziri huyo aliahidi kuyaweka
hadharani majina ya watu
wanaosafirisha dawa za kulevya
nchini, na alitekeleza ahadi hiyo
jana wakati akizungumza na
waandishi wa habari, kusema kuwa
watu hao wamenaswa baada ya
mfumo wa kamera (CCTV) za
uwanja huo kudaka matukio
kadhaa yaliyotokea siku ya tukio
hilo, kuanzia saa 9:25 hadi saa
10:30 alfajiri.
Ameagiza wafanyakazi hao wanne
pamoja na askari polisi mwenye
cheo cha koplo, mbeba mizigo na
mfanyabiashara aliyekuwa na
wasichana wawili waliokamatwa
Afrika Kusini, (ambao hatuwezi
kuwataja kutokana na kushindwa
kuwapata kujieleza) kuchukuliwa
hatua za kinidhamu, kukamatwa na
kuunganishwa na watuhumiwa
waliokwenda na mzigo huo Afrika
Kusini.
Mabegi hayo yaliyokuwa na dawa
za kulevya aina ya ‘Crystal
Methamphetamine’, yalipitishwa na
wasichana wawili wasanii
aliowataja kuwa ni Agnes Gerald
‘Masogange’ na Melisa Edward
ambao walidakwa siku hiyohiyo
katika Uwanja wa Ndege wa Oliver
Tambo, Afrika Kusini na tayari
wameshafikishwa mahakamani.
Juzi Dk Mwakyembe alifanya ziara
JNIA kukagua utendaji kazi kwenye
uwanja huo ikiwa ni siku tatu
baada ya ahadi aliyotoa akiwa
Mwanza kwamba katika kipindi cha
wiki mbili, atahakikisha
anawakamata vigogo wote walio
katika mtandao wa usafirishaji na
uingizaji wa dawa za kulevya
kupitia viwanja vyote vya ndege
nchini.
Saa nane baada ya ziara hiyo,
Maofisa wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege wanadaiwa kumkamata
Edwin Monyo akiwa na kete 86 za
dawa aina ya heroini na misokoto
34 ya bangi aliyokuwa akiisafirisha
kwenda Italia kupitia Zurich.
Mpango ulivyosukwa
Alisema siku ya tukio saa 9:28
kamera hizo za usalama
zilimwonyesha mbeba mizigo wa
uwanja huo akiwa
anazungukazunguka eneo la
kuingilia abiria kama mtu ambaye
ana ahadi na kukutana na mtu
fulani.
“Kamera pia zilimnasa ofisa
mwingine wa TAA kwa mara kadhaa
akitoka na kuingia ndani ya jengo
la abiria huku akizungumza na
simu, kitendo ambacho
hakiruhusiwi kabisa kwa
wafanyakazi wa eneo la ukaguzi wa
abiria,” alisema na kuongeza;
“Wakati huohuo, kamera zilikuwa
zinamwonyesha askari polisi
anayetuhumiwa kuhusika katika
mpango huo akiwa anarandaranda
eneo la uhakiki wa hati za kusafiria
kama vile anasubiri kitu fulani.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑