SHAHIDI KESI YA WEMA AGEUKA BUBU GHAFLA

image

KESI inayomkabili staa wa filamu
Bongo, Wema Isaac Sepetu ya
kudaiwa kumtukana matusi ya
nguoni na kumpiga vibao meneja
wa hoteli, Goodluck Kayumbu ilizua
kituko baada ya shahidi kugeuka
‘bubu’ ghafla.
Kituko hicho kilijiri Agosti 20,
mwaka huu katika Mahakama ya
Mwanzo Kawe jijini Dar ambako
kesi hiyo inaunguruma.
Mmoja wa makarani wa mahakama
hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake,
alisema kitu kilichoonekana kituko
ni pale shahidi wa mwisho
aliposhindwa kutoa ushahidi baada
ya sauti kukauka ghafla.
“Mlalamikaji alifika hapa na
mashahidi wake watatu, Boniface
Mati, Taito Osa na Melao ambapo
wawili walitoa ushahidi lakini Taito
alishindwa kutoa ushahidi wake
kwani sauti ilikata ghafla na ndipo
hakimu Bernice akamuamuru
anyamaze na kupanga tarehe
nyingine ya kuwasikiliza mashahidi
hao,” alisema karani huyo.
Mlalamikaji wa kesi hiyo,
alipoombwa na paparazi wetu
azungumzie ‘ ishu’ ya shahidi wake
kushindwa kuzungumza alisema
amekubaliana na uamuzi wa
mahakama na anasubiri tarehe ya
kurudi mahakamani ambayo ni
Septemba 30, mwaka huu.

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑