HII NI NOMA, WANAFUNZI NCHINI LIBERIA WAFELI WOTE MTIHANI WA KUJIUNGA NA CHUO. HAKUNA ATAYEJIUNGA NA CHUO. SOMA HAPA

image

Kwa mara ya kwanza katika historia
ya Liberia, wanafunzi wote
wamefeli mtihani wao wa mwisho
wasekondari na hivyo kumaanisha
kuwa hakuna hata mmoja ambaye
atafuzu kuingia chuo kikuu.
Waziri wa elimu wa Liberia
amesema ameshinda kufahamu ni
kwa nini hakuna wanafunzi hao
wamefeli kiasi hicho.
Zaidi ya wanafunzi elfu ishirini na
watano walianguka mtihani huo
ambao ungewapa fursa ya kujiunga
na chuo kikuu cha Liberia ambacho
ni moja ya vyuo vikuu
vinavyoendesha na serikali.
Lakini wasimamizi wa chuo hicho
wameiambia BBC kuwa wanafunzi
hao hawakuwa makini na ufahamu
mzuri wa lugha ya Kiingereza
ambayo ilitumiwa kuwatahini.
Taifa la Liberia linaendelea
kujinasua kutokana na athari za
mapigano ya wenyewe kwa
wenyewe yaliyomalizika zaidi ya
miaka kumi iliyopita.
Rais wa Liberia, Ellen Johnson
Sirleaf, ambaye pia ni mshindi wa
tuzo ya amani ya Nobel, amekiri
kuwa mfumo wa elimu nchini humo
bado ungali duni na unahitaji
marekebisho ya dharura.
Mwandishi wa BBC mjini Monrovia,
anasema shule nyingi nchini humo
havina vifaa vya kimsingi na
waalimu waliohitimu.
Lakini hii ni mara ya kwanza katika
historia ya taifa hilo kwa wanafunzi
wote kufeli mtihani huo licha ya
kulipa ada ya usajili ya dola
ishirini na tano.
Chuo hicho kikuu ambacho kina
idadi kubwa ya wanafunzi
hakitakuwa na wanafunzi wa mwaka
wa kwanza wakati muhula mpya
utakapoanza mwezi ujao.
Lakini wanafunzi wengi wanasema
hawajaamini matokeo ya mtihani
huo na waziri wa Elimu Etmonia
David-Tarpeh, ameiambia BBC kuwa
anatarajia kukutana na wasimamizi
wa chuo hicho ili kujadili suala
hilo.

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑