Wanigeria wanavyosota na kushindia mikate Bongo

image

Timu hiyo iliyowasili nchini Julai 7
mwaka huu, mbali na sakata la hoteli
pia wanatakiwa kuongeza dola 50
kwenye kila tiketi ya Shirika la Ndege
la Ethiopia ili waruhusiwe kurudi
kwao kwani walichelewa kuahirisha
safari hapo awali, walikuwa
waondoke kurudi Lagos Agosti 14
KUNA timu inaitwa 3Pillars ya
Nigeria. Ilitua kwa mbwembwe jijini
Dar es Salaam lakini baadaye
ikakiona cha moto na mpaka sasa
inasota.
Wachezaji wake wanateseka kwa kila
hali na pengine wakiondoka kwenye
ardhi ya Dar es Salaam huenda
wasirudi tena wala wasitake japo
kusikia neno Tanzania.
Wamekwama kuondoka nchini
kutokana na deni kubwa
wanalodaiwa kwenye Hoteli ya
Itumbi Magomeni waliyofikia siku 52
zilizopita. Wachezaji hao kwa sasa
wanalala wanne kwenye kila chumba
huku wakishindia maji na mikate.
Hali hiyo imesababisha Ubalozi wa
Nigeria nchini kuingilia kati na
kuanza harakati za kuwanusuru
tangu wikiendi iliyopita.
Timu hiyo iliyowasili nchini Julai 7
mwaka huu, mbali na sakata la hoteli
pia wanatakiwa kuongeza dola 50
kwenye kila tiketi ya Shirika la Ndege
la Ethiopia ili waruhusiwe kurudi
kwao kwani walichelewa kuahirisha
safari hapo awali, walikuwa
waondoke kurudi Lagos Agosti 14 .
Mpaka sasa wameshindwa kulipa
dola hizo 50 kila mmoja.
Kabla ya kuja nchini timu hiyo
ilifanya mawasiliano na Kampuni ya
SportLink ambayo ilipaswa
kuwagharimia kila kitu ikiwamo
malazi na chakula muda wote
watakapokuwa nchini na wao
kujilipia usafiri na vibali vya
uhamiaji.
Kampuni hiyo inayomilikiwa na
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga,
Selestine Mwesigwa, ililipa dola
2,000 kwa ajili ya malazi na chakula
kwa siku za awali.
Hata hivyo, Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) liliikatalia kampuni
hiyo kuratibu mechi za kimataifa kwa
madai kuwa haina vigezo.
Baada ya hapo Chama cha Soka Dar
es Salaam (DRFA) kikachukua jukumu
la kuandaa mechi ambapo nao
walikikabidhi Chama cha Soka cha
Temeke (Tefa) jukumu hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Tefa, Saleh
Ndonga alisema: “Tuliogopa kuratibu
mechi za hiyo timu kwa kuwa tulijua
kwamba timu hiyo ilikuwa si ya
halali kabla ya kuhakikishiwa na TFF
hivyo tukatafuta mratibu kusimamia
ili Tefa iepukane na hasara.
“Mapato kwenye mchezo dhidi ya
Yanga yalikuwa ni Shilingi milioni 28
kwa mujibu wa ripoti ya Mratibu,
Jerry Maganga hivyo mratibu huyo
alituambia kuwa aliwapa Yanga
Shilingi milioni 11 na 3 Pillars
walipaswa kuwapa Shilingi milioni
5.7 lakini akadai hakuwapa kwa
sababu alikuwa amepata hasara
kubwa kutokana na kuandaa mchezo
dhidi ya Simba na ikagoma kutokea
uwanjani dakika za mwisho,” alisema
Ndonga.
Baada ya mechi na Yanga
walikwenda Tanga kucheza na
Coastal Union (walitoka suluhu) na
siku iliyofuata waratibu walitaka
wacheze mechi nyingine dhidi ya
Tanga All Stars, Wanigeria wakagoma
kwa madai kuwa wamechoka na
kwamba haikuwa haki.
source-mwanaspot

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑