WALIOFUKUZWA TAZARA WAREJESHWA

image

Mkutano wa bodi ya Mamlaka ya
Reli Tanzania na Zambia
(Tazara) ,imetengua maamuzi ya
kuwafukuza wafanyakazi 1,067 na
kuagiza warudishwe kazini, agizo
hilo linamtaka kila mfanyakazi
kuendelea na kazi huku mishahara
ikishughulikiwa. Mkurugenzi Mkuu
wa Tazara, Ronald Phiri, alisema
jana pasipo kutaja sababu kuwa
yeye aliagizwa na bodi kutangaza
kurejea kwa wafanyakazi hao kama
alivyotangaza awali kufukuzwa
kwao.
“Siku mbili zilizopita nilitangaza
wafanyakazi 1,067 niliwafukuza
kazi, lakini leo natangaza warudi
kazini na kuendelea na kazi,”
alisema Phiri na kuongeza kuwa
hatua hizo zimechukuliwa kwa kuwa
hakuna mfanyakazi aliyepewa barua
ya kufukuzwa na kuhesabika kuwa
bado ni wafanyakazai wa Tazara.
Mwenyekiti wa Chama cha
Wafanyakazi wa Reli Tanzania
(Trawu), Mussa Kalala, alisema
hakuna mfanyakazi atakayerudi
kazini hadi mishahara
itakapolipwa.
Alisema kuwa wataweza kurudi
ikiwa wajumbe wa bodi watafika
Tazara na kuzungumza na
wafanyakazi.
HABARI NA LEONCE ZIMBANDU
CHANZO: NIPASHE

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑