WABONGO CHINA WAHENYESHWA

image

Taifa la China halina mzaha
mbele ya biashara haramu ya
madawa ya kulevya na kwa
kutambua kwamba wanaohusika
zaidi ni Waafrika , sasa hivi kila
mja mwenye ngozi nyeusi
aliyepo nchini humo, anapewa
msoto wa nguvu .
Wabongo wanaoishi China, kwa
sasa wanahenyeshwa isivyo
kawaida katika msako uliopewa
jina
na Watanzania kwamba ni
Oparesheni Safisha Wauza
Unga.
Katika hoteli wanazofikia, vijiwe
vyao, barabarani na kadhalika,
kote huko wanapewa msoto wa
guvu kwa kile kinachoelezwa
kuwa Wachina hawana imani
tena na Watanzania na
Waafrika kwa jumla ama
wanaoishi nchini humo au hata
wale wanaoingia na kutoka.
“Wazungu wa unga
(wafanyabiashara wa madawa ya
kulevya) wanatuharibia starehe
hapa China, hatuishi kwa amani
tena. Mtu unaweza kukaguliwa
siku nzima kisa eti
wanawatafuta wanaouza unga ,”
alisema Artides Kimota ambaye
ni Mtanzania anayeishi China
kwa sasa.
Aliongeza: “Unajua sasa hivi
China imekuwa na uingizwaji
mkubwa wa madawa ya kulevya.
Kwa Serikali ya China hii ni
kashfa nzito . Kwa vile wanajua
Waafrika ndiyo sababu kuu,
sasa hivi kila Mwafrika anapewa
msukosuko .
“ Kwa kweli ukiwa Mwafrika
hapa China ni mateso makubwa
sana kwa sasa. Kuna agizo la
serikali ambalo limelitaka jeshi
la polisi hapa China
kuhakikisha madawa ya kulevya
yanatokomezwa na wahusika
wanakamatwa.
“Kila anayekamatwa na madawa
ya kulevya au na kitu chochote
ambacho siyo halali ,
anafunguliwa mashtaka . Mimi
naishi kwenye Jiji la Qingyuan,
nimeshahuhudia Mtanzania
mmoja, Wanigeria wawili na
Waghana watatu wakikamatwa.
“Kote hakuna kupumua, hata
huko Guangzhou, Beijing na
kwingineko kunatisha kwa
msako. Nasikia kwenye Mji wa
Shanwei alikamatwa Mtanzania
mwingine, akakutwa na
ungaunga wa marumaru ambao
alikuwa nao kama sampuli kwa
ajili ya biashara zake,
alikamatwa lakini aliachiwa
baada ya kupimwa na
kugundulika siyo madawa ya
kulevya.”
Habari zaidi zinasema kuwa
pamoja na sifa mbaya ya
Watanzania nchini humo lakini
imebainishwa kwamba
Wanigeria ndiyo kundi hatari na
wanawindwa zaidi kwa sababu
raia wa nchi hiyo
wameshachafuka sana .
Imebainishwa zaidi kuwa kwa
vile siyo rahisi kumtofautisha
Mnigeria na Waafrika wengine
kwa haraka , ndiyo maana kila
Mwafrika anapoonekana ni
lazima ale msoto wa kukaguliwa
ili kuhakikisha kama ana ‘mzigo’
au hana .
Risasi Jumamosi linamiliki picha
zinazowaonesha baadhi ya
Waafrika wakiwa chini ya ulinzi,
wakitembezwa vifua wazi,
kueleka vituo vya polisi
kufunguliwa mashtaka ya
uhalifu mbalimbali ikiwemo
madawa ya kulevya.
KINACHOWAPONZA NI HIKI
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
China, taifa hilo limeshtukia
kwamba pamoja na sheria kali
za udhibiti wa madawa ya
kulevya zilizopo na adhabu kali
ikiwemo ile ya juu kabisa ya
kunyongwa hadi kufa kwa mtu
anayekutwa na hatia ya
kujihusisha na biashara hiyo ,
polisi wameendelea kupigwa
bao la kisigino .
Imeelezwa kwamba watu
wanaosafiri na madawa ya
kulevya tumboni , maarufu kama
punda ndiyo wanaofanya
madawa yazagae nchini humo.
“Punda ndiyo wanatuponza ,
Serikali ya China imeshtukia
kuona kwamba madawa yapo
sana mitaani, kwa hiyo
kukomesha kabisa hilo,
wanafanya msako hatari sana .
Wakifika chumbani kwako
utajuta, wanapekua kila upande
wa chumba .
“Vilevile ikitokea mtu anawasili
uwanja wa ndege akiwa dhaifu ,
anafuatiliwa sana. Asikwambie
mtu, hakuna Mwafrika aliyepo
China anayeishi kwa raha , iwe
unauza au huuzi lazima
uhenyeshwe, ” alisema Dominick
Rafiki anayeishi Guangzhou,
China.
CHINA YASISITIZA KUENDELEA
KUNYONGA
Ripoti ya Shirika la Haki za
Binadamu la Amnesty
International mwaka 2012 ,
iliitaja China kama taifa kinara
kwa kunyonga watu wenye
makosa mbalimbali na kuitaja
nchi hiyo kama katili zaidi
duniani.
Amnesty International
inapingana na adhabu ya kifo ,
kwa hiyo imekuwa ikitumia
jitihada mbalimbali kuhakikisha
linaishawishi China iachane na
hukumu za kunyonga watu bila
mafanikio.
Shirika hilo lilieleza kwamba
China imeendelea kuweka
msisitizo wa kunyonga watu ,
huku ikiwa na rekodi ya
kunyonga maelfu ya watu kila
mwaka.
BALOZI AKIRI HALI NI MBAYA
Balozi mpya wa Tanzania nchini
China, Luteni Jenerali Mstaafu,
Abdulrahman Shimbo amekiri
kwamba hali ni mbaya kutokana
na wimbi kubwa la Watanzania
kukumbwa na kashfa ya
madawa ya kulevya, huku
wengine wakiwa
wameshahukumiwa kunyongwa.
“Ni kweli hali ni mbaya, kuna
vijana wetu wengi wanaipa sifa
mbaya nchi yetu hapa . Kama
inavyofahamika, mimi bado
mgeni lakini nikipewa muda
kidogo nitakuwa na ripoti kamili
ya jinsi Watanzania
wanavyohusishwa na hii
biashara haramu ya madawa ya
kulevya,” alisema Balozi Shimbo
ambaye alikuwa Mnadhimu wa
Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ )

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑