Uwezo wa Kaseja wamshtua kocha Stars

image

KOCHA wa makipa wa kikosi cha
Taifa Stars, Juma Pondamali ,
ameshangazwa na uwezo wa
kipa wake namba moja, Juma
Kaseja, licha ya kutokuwa na
klabu yoyote kwa sasa .
Kaseja ambaye tangu
alipotemwa na Simba
hajafanikiwa kupata timu ,
alimjumuishwa katika orodha ya
kikosi cha Stars kilichopo
kambini kikijiandaa na mchezo
dhidi ya Gambia utakaopigwa
Jumamosi ijayo jijini Banjul ,
Gambia.
Akizungumza na Championi
Jumatatu, Pondamali amesema
tangu kikosi hicho kianze
mazoezi mwishoni mwa wiki
iliyopita, Kaseja ameonyesha
uwezo mkubwa wa kudaka huku
akiwazidi baadhi ya makipa
wenzake ambao wametoka
katika michezo ya Ligi Kuu Bara.
Pondamali ambaye ni kipa wa
zamani wa kikosi hicho cha
Stars, amesema mbali na uwezo
huo wa Kaseja, pia kipa huyo
na nahodha wa kikosi hicho,
ameonyesha kuwa mwepesi ,
jambo ambalo linaashiria
alikuwa akijifua vizuri.
“Hajaonyesha tofauti yoyote
mpaka sasa tangu ajiunge na
timu, niliwapa mazoezi kadhaa
tofautitofauti lakini Kaseja
alifungwa mabao mawili huku
wengine wakifungwa sita, kitu
ambacho kilinishangaza ,
nikawauliza wenzake kwa nini
wanafanya vibaya kuliko Kaseja ,
wakanijibu wana uchovu wa
safari,” alisema Pondamali .
“Ukiacha hilo, pia bado
ameonekana mwepesi zaidi ,
ukiwa nje ya timu mara nyingi
tunahofia unaweza kuongezeka
uzito kutokana na kutokuwa na
ratiba ya kutosha ya mazoezi ,
lakini Kaseja ameonekana kuwa
sawa, inaonyesha alikuwa
akijifua kwa mazoezi binafsi ,”
aliongeza.
Kaseja alikuwa amekaribia
kujiunga na FC Lupopo ya DR
Congo lakini dili hilo likafa
kutokana na baadhi ya watu
kudaiwa ‘ kumchomea utambi

posted by janjaweed!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑