BAADA YA KUFUNGWA NA GAMBIA – KIM POULSEN ASEMA TAIFA STARS ILISTAHILI KUFUNGWA

image

Taifa Stars imemaliza vibaya mechi
za mchujo za Kombe la Dunia,
Kanda ya Afrika baada ya kufungwa
na Gambia huku Kocha Kim Poulsen
akisema timu yake imefungwa
mabao mepesi.
Wenyeji Gambia wameshinda
mabao 2-0 katika mechi hiyo
iliyochezwa leo (Septemba 7 mwaka
huu) kwenye Uwanja wa
Independence ulioko hapa jijini
Banjul ukiwa ni ushindi wake wa
kwanza katika kundi hilo la C
ambapo imemaliza ikiwa ya mwisho
ikiwa na pointi nne.
Akizungumza baada ya mechi hiyo,
Kocha Poulsen amesema Gambia
ilistahili kushinda kwa vile
ilitengeneza nafasi nyingi kuliko
timu yake, na kuongeza kuwa
mabao iliyopata Gambia yalikuwa
mepesi.
“Hatukutengeneza nafasi nyingi za
kufunga, lakini tukaruhusu mabao
mapesi. Nawapongeza Gambia
kwani walistahili ushindi.
Unapofanya makosa unaadhibiwa.
Gambia ilikuwa timu nzuri leo,
kwani ilitengeneza nafasi nyingi za
kufunga, sisi tukatoa mabao
mepesi,” amesema Kim.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager
imemaliza katika nafasi ya tatu
katika kundi hilo lililokuwa na timu
nne ikiwa na pointi sita ilizozipata
nyumbani kwa kuzifunga Morocco
na Gambia.
Hata hivyo, Kim amesema sababu
nyingine ya kutofanya vizuri ni
kuwakosa wachezaji wanaocheza
nje ya nchi na wengine wa kikosi
cha kwanza ambao ni majeruhi.
Mabao yote ya Gambia katika mechi
hiyo iliyochezeshwa na Munyemana
Hudu kutoka Rwanda yalifungwa na
nahodha wa timu hiyo Mustapha
Jarjue. Alifunga la kwanza dakika
ya 44 na kupachika lingine dakika
ya 51, mabao yaliyotokana na
wachezaji wa Stars kutokuwa
makini.
Katika mechi hiyo Stars
iliwakilishwa na Juma Kaseja,
Vincent Barnabas, Erasto Nyoni/
David Luhende, Nadir Haroub,
Henry Joseph, Frank Domayo,
Haruni Chanongo, Amri Kiemba,
Mrisho Ngasa, Simon Msuva na
Khamis Mcha/Juma Liuzio.
Taifa Stars inaondoka Banjul kesho
(Septemba 8 mwaka huu) saa 6
mchana kwa ndege ya Arik hadi
Dakar, Senegal ambapo
itaunganisha kwa ndege ya Kenya
Airways kupitia Nairobi ambapo
itawasili Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
keshokutwa (Septemba 9 mwaka
huu) saa 8.05 mchana.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑