BABU MNYARWANDA AJINYONGA KUKWEPA KUREJESHWA RWANDA

image

-Achanachana mamilioni ya noti za
TZ
-Aliingia nchini 1976, mkewe
atoweka
Raia wa Rwanda amejinyonga kwa
kamba chumbani kwake, tukio
linalohusishwa na zoezi
linaloendelea hivi sasa nchini la
kuwasaka wahamiaji haramu na
kuwarejesha makwao.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo
la tukio, marehemu anatajwa kuwa
ni Francis Mathias (75), ambaye
alikuwa mkazi wa kitongoji Kikukuru
kata Kikukuru, tarafa Mabira wilayani
Kyerwa mkoani Kagera.
Mwenyekiti wa kitongoji cha
Kikukuru, Joseph Leo, jana
alilithibitishia NIPASHE kutokea kwa
tukio hilo na kuwa alipata taarifa
hizo kutoka kwa binti wa marehemu
juzi saa 3:00 asubuhi.
“Baada ya kupata hizo taarifa
niliongozana na mgambo, tulipofika
mlango wa chumba chake ulikuwa
umefungwa kwa ndani, tukafanikiwa
kuuvunja tukaingia ndani na kukuta
amejitundika kwa kamba,” alisema
Leo na kuongeza kuwa marehemu
alikuwa mfugaji na mkulima.
Alisema kuwa kabla ya kujiua, mzee
huyo alichana fedha za Kitanzania
zinazokadiriwa kufikia Shilingi
milioni saba zikiwamo noti za Sh.
5,000 na za Sh. 10,000, ambazo
zilikutwa ndani ya chumba chake.
Leo alisema baada kushuhudia
alipiga simu kwa Ofisa Mtendaji wa
Kata Kikukuru ambaye alifika na
kupiga ngoma na watu walikusanyika
kushuhudia kilichotokea na baadaye
kwenda kutoa taarifa katika kituo cha
Polisi.
Alipotakiwa na NIPASHE kuthibitisha
kama kweli mwananchi wake
aliyejinyonga alikuwa raia wa
Rwanda, Leo alithibitisha na
kufafanua kuwa tayari alikwisha
kumuorodhesha kwa lengo la
kurejeshwa kwao katika opereshani
iliyoanza Jumamosi ya kuwarejesha
makwao wahamiaji haramu wanaoishi
mkoani Kagera.
Aliongeza kuwa aliwahi kumhoji
marehemu Mathias ambaye
alimweleza kuwa alikuja Tanzania
kutoka Rwanda tangu mwaka mwaka
1976.
Naye Ofisa Tarafa ya Mabira,
Nicolaus Rugemalira, alisema
uchunguzi wa awali wa kimazingira
umeonyesha kuwa kulikuwa na
mgogoro wa familia baada ya
marehemu kutaka wauze mali zao
zote warudi Rwanda, lakini familia
yake haikukubaliana naye kutokana
na mkewe kuwa raia wa Tanzania.
“Mke wake ni Mtanzania, inaonekana
baada ya familia yake kukataa
uamuzi wake wa kuuza mali zote ili
waondoke, aliamua kuchukua uamuzi
huo,” alisema Rugemalira.
Akizungumzia tukio hilo, binti wa
marehemu, Melania Francis,
alithibitisha kuwapo ugomvi kati ya
baba yake na mama yake hali
iliyosababisha mama yao kuondoka
bila kufahamika alikoelekea.
Alisema siku ya tukio aliamka na
kuwaandaa wadogo zake kwenda
shuleni na baada ya hapo alikwenda
shambani kuona kama vibarua
wameanza kazi ya kulima, lakini
aliporudi nyumbani alishangaa
kuona mlango wa chumba cha baba
yake bado umefungwa wakati
haikuwa kawaida yake kulala hadi
saa moja.
Melania alisema alibisha hodi bila
majibu, akajaribu kufungua
ikashindikana na alipochungulia
aliona fedha nyingi zimetapakaa
ndipo alipokimbia kutoa taarifa kwa
mwenyekiti wa kitongoji.
“Nafahamu baba alikuwa na uwezo
wa kumiliki fedha hizo, lakini
sikufahamu anazihifadhi wapi,”
alisema binti huyo wa marehemu.
Alisema wamezaliwa watoto watano
katika familia hiyo na kwamba ndugu
zake wawili walitoweka na kubakia
watatu na kuongeza kuwa kuwa
anatambua kuwa baba yake alikuwa
raia wa Rwanda.
Alipotakiwa kueleza kama anafahamu
alikoelekea mama yake, binti huyo
alidai kuwa hafahamu ingawa
anafahamu kuwa ni mzaliwa wa
Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera.
Kutokana na kutoweka kwa mama
huyo pamoja na wanafamilia
wengine, uongozi wa eneo hilo
unaendelea na ufuatiliaji ili kujua
wanafamilia wengine wamekwenda
wapi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera,
Philip Kalangi, akizungumza kwa njia
ya simu jana, alisema kwa sasa yuko
katika operesheni inayoendelea ya
kuwasaka wahamiaji haramu na kuwa
angefuatilia taarifa hizo baadaye
baada ya kuwasiliana na watendaji
walioko chini yake.
MAOFISA UAHAMIAJI FEKI MBARONI
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam
linawashikilia watuhumiwa wanane
wanaojifanya maofisa wa Idara ya
Uhamiaji na kupora mali kwa
wananchi katika maeneo ya
Mwananyamala.
Kamanda wa wa Polisi Kanda
Maalum, Suleiman Kova, alisema,
polisi walifanya msako mkali
unaoendelea na kufanikiwa
kuwakamata vijana wanane juzi.
Kova alisema vijana hao waliojifanya
maofisa uhamiaji waliingia katika
nyumba za raia wa Malawi wanaoishi
Mwananyamala kwa kuwajeruhi kisha
kuwapora mali zao.
Kova aliwataja watuhumiwa hao
kuwa ni Amos Rabus (31), mkazi wa
Mwananyamala; Jeremiah Thomas
(21), mkazi wa Mbezi; Paulo Punjo
(24), mkazi wa Kimara na Kamarada
Innocent (35), mkazi wa
Mwananyamala pamoja na wengine
wanne ambao walijifanya ni maofisa
uhamiaji.
RC DAR: AIBUA MAPYA
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Said Meck Sadiki, amesema
kuna baadhi ya shule jijini Dar es
Salaam zinazojiita ni za kimataifa na
zinawatumia walimu wasio na vibali
vya kuishi na kufanya kazi nchini.
Alisema kuwa walimu 16 kutoka
baadhi ya shule jijini Dar es Salaam
walikutwa bila kuwa na vibali vya
kuishi nchini wala kufundisha.
Wakati huo huo, Ofisa Uhamiaji wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Grace
Hokororo, amewapa siku saba
wahamiaji haramu wote
wajisalimishe.
Alisema kati wahamiaji haramu 465
waliokamatwa, 108 wamerejeshwa
makwao na wengine wamepewa
muda ili kuondoka.
Agizo la kuwataka wahamiaji haramu
kuondoka nchini lilitolewa na Rais
Jakaya Kikwete Julai mwaka huu
akiwa ziarani Mkoa wa Kagera.
Baadaye, Waziri wa Mambo ya Ndani,
Dk. Emmanuel Nchimbi, alitoa tamko
kwa wahamiaji haramu la kuwataka
kurejea makwao mara moja kwa
hiyari, kwani zoezi la ghafla la
kuwasaka na kuwarejesha lingeanza
wakati wowote kuanzia wakati huo.
CHANZO: NIPASHE, JUMATANO
SEPTEMBA 11, 2013

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑