MASOGANGE AANGUSHIWA PATI BONGO!

image

WAKATI msanii Agnes Gerald
‘Masogange’ akihenyeka nchini Afrika
Kusini kwa kesi ya madawa ya
kulevya, hapa Bongo baadhi ya
mashosti zake wakiongozwa na
Jacqueline Wolper hivi karibuni
walimfanyia pati.
Pati hiyo ambayo waalikwa wengi siyo
mastaa walikunywa, wakala na
kucheza muziki, ilikuwa ya
kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa
Masogange ila kiwanja ilipofanyikia
ilifanywa siri.
Mmoja wa watu waliohudhuria
sherehe hiyo aliyeomba hifadhi ya
jina lake alilitonya gazeti hili kuwa
pati hiyo haikuwa na mualiko wa
watu wengi lakini ilifana huku keki
kubwa ikiwa imetolewa na Wolper na
kuandikwa; Happy Birthday
Masogange, from da best Wolper.
“Ilikuwa ni pati ya kiaina, watu
walishangweka kiaina ila kuna wakati
walionyesha nyuso za simanzi pale
walipokumbuka kuwa mhusika yuko
kwenye matatizo. Ingenoga zaidi
angekuwepo lakini ndiyo hivyo tena,
Mungu atamsaidia,” alisema mtoa
habari huyo.
Katika kuonesha sherehe ilivyokuwa,
Wolper kupitia ukurasa wake wa
Instergram alitupia picha ya hafla
hiyo na kuwafanya baadhi ya wadau
kushangaa kwani hawakutarajia
kufanyika kwa pati hiyo bila ya
uwepo wa mwenzao.
Mwandishi wetu alifanya jitihada za
kumpata Wolper kupitia simu yake
ya mkononi ili aizungumzie pati hiyo
lakini hakuweza kupatikana.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑