Mbwana, Mkwanda wamliza Matumla

image

TAARIFA za kukamatwa na unga kwa
mabondia wawili wa familia maarufu
ya mchezo wa ngumi nchini ya
Matumla, zimezua kilio na gumzo.
Mbwana Matumla ambaye ni
mkubwa, ameelezwa kukamatwa
mpakani mwa Uswiss na Ujerumani
wakati Mkwanda Matumla
amekamatwa Addis Ababa nchini
Ethiopia.
Rashid ambaye ni kaka wa Mbwana
na Mkwanda, amesema bado wapo
katika hali ya kutoelewa
kinachoendelea.
“Tumesikia Mkwanda hadi ubalozi wa
Tanzania nchini Ethiopia
umethibitisha, lakini Mbwana bado
hatuna uhakika ingawa hakuna
anayeweza kumpata kwa sasa.
“Unajua Mbwana hakumuaga hata
mkewe, kweli inatusikitisha sana na
tunasikia maumivu makubwa.
“Kama kweli itakuwa ni hivyo, basi
watakuwa wameiangusha sana
familia ambayo ilipigana kujenga
jina. Lakini hatuwezi kuwatenga kwa
kuwa ni ndugu zetu, tutawapigania,”
alisema Matumla akionyesha
kusikitishwa.
Mkwanda ambaye alikuwa anaishi
nchini Sweden, alikamatwa kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Bole jijini Addis Ababa, Ethiopia
akiwa na mwanasoka wa zamani,
Joseph Kaniki ‘Golota’ aliyewahi
kuzichezea Simba, Mtibwa Sugar,
Rayon Sports ya Rwanda na timu ya
taifa, Taifa Stars.
Maisha:
Mkwanda alikuwa akiishi nchini
Sweden ambako alikuwa na mpenzi
wake aliyejaaliwa naye kupata mtoto
mmoja aitwaye Liam aliyezaliwa
mwaka 2010.
Mpenzi wake huyo raia wa Sweden
alikuwa mwanafunzi katika chuo
kimoja mjini Norrkoping wakati
Mkwanda alikuwa mwanafunzi katika
chuo kingine akisomea Lugha ya
Kiswidi.
Kurejea:
Hivi karibuni inaelezwa alirejea jijini
Dar es Salaam na alionekana ni mtu
mwenye furaha na mishemishe
kibao.
Alikuwa anamiliki gari aina ya Toyota
Vitz ambalo pia aliliuza lakini kuna
taarifa kuwa, alinunua kiwanja katika
moja ya maeneo ya Jiji la Dar.
Ngumi:
Katika familia ya Matumla, Mkwanda
ndiye alikuwa bondia mdogo kuliko
wote baada ya wengine sita.
Mkubwa ni Ally ambaye ni
marehemu, anafuatiwa na Rashid
Matumla aliyewahi kuwa bingwa wa
dunia mara mbili, bingwa wa
mabara, Afrika mara moja na ndiye
anaaminika kuwa bondia mkali zaidi
ya wengine.
Anafuatia Hassan, Mbwana ambaye
anaelezwa ‘kudakwa’ Ulaya, Kareem
na Mkwanda.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑