MWIMBAJI AMSHUSHUA MASHAUZI

image

MWIMBAJI nyota wa muziki wa
mwambao anayepiga kazi Kundi la
King’s Modern Taarab la jijini Dar es
Salaam, Aisha Vuvuzela
amemshushua bosi wake wa zamani,
Isha Ramadhani ‘Mashauzi’ kwa
kumwelezea kuwa ana gubu.

image

Akihojiwa na kituo cha redio cha
Planet cha mkoani hapa katika
Kipindi cha Mirindimo ya Pwani,
Aisha alisema alishawahi kukaa zaidi
ya miezi sita bila kusalimiana
mkurugenzi huyo wa Kundi la
Mashauzi Classic Modern Taarab.
“Huwezi kuamini, nilikuwa nakaa
miezi sita bila kuchangamkiana na
lsha, kisa hapendi mwanamuziki
wake apendeze, mfano unaweza
kuvaa nguo nzuri mitaani kila mtu
anakusifia umependeza, ukienda
kazini lsha anakuambia vua nguo
hiyo umechukiza,” alisema mwimbaji
huyo wakati wa kipindi hicho
kinachoendesha na Watangazaji,
Rukia Ndege na Warda.
Aisha aliyejiunga King’s akitokea
Mashauzi Classic, alisema kabla ya
kuanza kuimbia bendi hiyo, alikuwa
akipiga shoo katika vigodoro kwa ajili
ya kujipatia pesa ya kula.
Akisimulia historia yake kwa ufupi,
mwimbaji huyo alisema aliwahi
kuolewa na kuzaa mtoto mmoja wa
kiume aitwaye Othman kabla ya
kutengana na mumewe.
“Kwa sasa sina mume wala
mchumba, niko free na mume
atakayenioa akubaliane na masharti
yangu ya kuendelea kuimba taarab,”
alisema.
Msanii huyo alifika mjini hapa
Ijumaa iliyopita saa 7 mchana na
kwenda moja kwa moja kwenye
studio za redio hiyo zilizopo Hoteli
ya Mount Uluguru ambako baada ya
kumalizika kwa kipindi, alirejea Dar
es Salaam.
Kipindi hicho cha kila siku huwa
kinaanza saa 8 mchana mpaka saa
10 jioni ambapo kwa muda wote huo,
Aisha alitumia nafasi hiyo kumchana
lsha Mashauzi.
Katika hatua nyingine paparazi wetu
aliyetinga ndani ya studio hizo
alishuhudia kituko kingine cha
mtangazaji wa kipindi hicho, Bi.
Rukia Ndege ’Mama wa Misuri’
akimseti nywele Aisha ndani ya
stundi hiyo wakati alipokuwa
akihojiwa na Warda.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑