NAPE: CHADEMA WAMEPEWA MABILIONI TOKA NJE KUVURUGA MCHAKATO WA KATIBA

image

Nape Nnauye Katibu wa
halmashauri kuu ya CCM (NEC)
Itikadi, Siasa na Uenezi
akiwahutubia wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika
mjini Kahama jana.
Adai ndio chanzo cha kupigana
bungeni
Asema ndizo walizotumia
kuzunguka na helkopta nchini.
Aeleza yaliyotokea bungeni sio
bahati mbaya, Chadema
waliyapanga
Ashukuru bunge kuendelea
kuonyeshwa”live” ili wananchi
waone ujinga wao.
Awatuhumu kuweka masilahi
yao mbele badala ya nchi.
Asisitiza CCM kuendelea
kuheshimu uamuzi wa wananchi
juu ya katiba.
Aonyesha madai ya Chadema
kitakwimu yasivyojali wakulima
na wafanyakazi.
Katibu wa NEC ya CCM itikadi na
Uenezi amesema kinachowasumbua
Chadema mpaka wanafanya yote
waliyoyafanya hasa ngumi na vurugu
bungeni ni namna watakavyoeleza
kwa waliowapa pesa za kuvuruga
mchakato wa katiba nchini kwani
wanatakiwa kupeleka mrejesho jinsi
walivyofanikiwa na jinsi walivyotumia
mabilioni hayo.
Nape ameyasema hayo kwenye
mkutano mkubwa wa hadhara mjini
Kahama kwenye ziara ya karibu siku
ishirini kanda ya ziwa kwa mikoa
mitatu yaani Shinyanga,Simiyu na
Mara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa
Ndg. Abralhaman Kinana.
“Wenzetu hawa nasikia wamepewa
mabilioni toka nje kwa kisingizio cha
kushiriki mchakato wa katiba, na
kama ilivyo kwa vibaraka wengine
katika bara la Afrika lengo la mapesa
hayo sio kuwawezesha kushiriki bali
kuanzisha fujo na vurugu ili
mchakato usimalizike salama iwe
ajenda 2015 kwani kimsingi hawana
ajenda mpya” alisisitiza Nape.
Akielezea swala la pesa kutoka nje
Nape alisema mara tu baada ya
rasimu ya kwanza kutoka Katibu
Mkuu wa Chadema alikwenda nje ya
nchi na akakaa kwa muda na
aliporudi tu, ndio Chadema
wakapanga kuanza kuzunguka na
helkopta.
“Babu atwambie alifuata nini nje?
Na pesa za kuzunguka na misafara
miwili tofauti ya helkopta walitoa
wapi? Na watwambie kama
walisharudisha mrejesho kwa
wafadhili wao” alisema Nape
Nape aliendelea kusisitiza kuwa yote
yaliyotokea bungeni si mambo
yaliyotokea kwa bahati mbaya
isipokuwa ni mambo yaliyopangwa na
Chadema katika mkakati wa kutimiza
moja ya malengo yao.Alisema ilikua
ni lazima watafute mahali pa
kufanya kituko bungeni ili iwe
mjadala na ili wapate sababu na
picha za kuonyesha kwa waliowapa
pesa kuwa wanapambana.
“hili walilofanya Chadema bungeni
ni jambo walilopanga katika mkakati
wao wa ‘civil
disobidiency’ …machafuko ya umma
dhidi ya dola, mkakati ambao
unaratibiwa kutoka nje na baadhi ya
wale waliokuwa wakoloni katika nchi
zetu za Afrika. Lengo ni kusababisha
machafuko na nchi kutotawalika”
alisema Nape.
Nape alisema ndio maana CCM
ilisisitiza lazima bunge liendelee
kuonyeshwa na televisheni ili
kuonyesha yanayoendelea bungeni
kuwawezesha wananchi kuona
kinachofanywa na wawakilishi wao.
“bila shaka wananchi mmeona
kilichotokea bungeni kwa macho
yenu, sina haja ya kuwaeleza.
Mmeona wabunge wa upinzani
walichofanya,uchaguzi ujao
tupunguze idadi ya vichaa bungeni
ili kodi zetu zitumike vizuri,kwani
tuliwatuma wakajadili maendeleo
yetu wao wamegeuza bunge uwanja
wa masumbwi.
Aidha Nape akifafanua hoja ya
upinzani bungeni juu ya idadi ya
wabunge wa bunge maalum la katiba
alisema upinzani hawana hoja ya
msingi bali wanasukumwa na
ubinafsi na ulafi wa madaraka.
“Hoja iliyowafanya wapigane bungeni
haina mashiko, wanataka idadi
iongezwe ya wabunge wa bunge la
katiba kutoka 357 mpaka 792. Hivi
nani anabeba mzigo huu wa
kuwalipa hawa wabunge kama sio
mwananchi wa kawaida? Halafu
mnajiita watetezi wa wanyonge?
Hamuoni aibu?” alihoji Nape.
Akiendelea kufafanua Nape anasema,
” katika hali ya kawaida
tungetegemea wajenge hoja ya kundi
kubwa katika jamii ya kitanzania
ambao ni wakulima na wafanyakazi
ndio wawe na uwakilishi mkubwa
kwenye hilo bunge kama tunataka
katiba kweli ya wananchi lakini
badala yake wao wanapendekeza
wawakilishi kutoka vyama vya siasa
ukiacha wabunge waliopo sasa wawe
72 na wakulima wawe 10 tu!
Wanataka katiba ya vyama vya siasa
badala ya katiba ya nchi kwa ajili ya
wananchi. Wanataka wafugaji wawe
10 tu na wafanyakazi 40. Kwa uwiano
wa kawaida asilimia 80% wa
wananchi wa nchi hii ni wakulima,
tungetegemea wangependekeza
idadi yao kuwa kubwa lakini wao
wanawapuuza wakulima na wafugaji
kwa kudai wawe kumi tu”!
Nape alimalizia kwa kudai kuwa siku
za vyama kama Chadema
zinahesabika maana hii ya katiba
ndio ilikuwa karata yao ya mwisho.
” Nimalizie kwa kuwatahadharisha
vijivyama hivi vingine kama CUF,
NCCR mageuzi na wengine kuwa
wenzao wamepewa mapesa wao
wanwaunga mkono kwa ajenda
iliyojificha. Na kwakuwa hili la
kuvuruga katiba ndio karata yao ya
mwisho basi tutarajie anguko baya
sana kwa Chadema na huo ndio
utakuwa mwisho wao”!alimalizia
Nape.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑