NJEMBA YAMKUTA MAZITO

image

NJEMBA moja iliyojulikana kwa jina la
Haji Bakari maarufu kama Mchome
limekamatwa baada ya kudaiwa
kutapeli kiasi cha shilingi 570,000
kwa njia ya simu za mkononi.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali,
njemba hilo lilifanikisha utapeli huo
kwa kutumia majina ya watu
wanaofahamiana na washirika
kibiashara.
Kijana huyo aliomba pesa hizo kwa
madai kuwa gari lake limemharibikia
maeneo ya Chalinze mkoani Pwani
hivyo alihitaji kiasi hicho ili aweze
kulitengeneza. Bila hiyana,
aliyeombwa alitoa fedha hizo kwa
moyo mmoja ingawa kwa awamu
mbili.
Akizungumza na gazeti hili, mtu
aliyetapeliwa aliyejitambulisha kwa
jina la Godilizen Moshi alisema
baada ya kumkamata mtu huyo,
alijihami na kusema kuwa aliyefanya
mchezo huo ni pacha wake.
Akisimulia mkasa huo, Moshi alidai:
“Kijana huyu ni mzoefu na alikuwa
akitumia simu nambari 0655 301646,
nilimuamini baada ya kunitajia jina
la mtu ambaye nafahamiana na
tunashirikiana kibiashara.”
Alisema baada ya kukamilisha
kumpatia kiasi hicho cha fedha
alizoomba alimpigia simu ili kuhakiki
kama amezipata lakini ilipopokelewa,
mpokeaji alisema alikuwa mazishini
mkoani Kilimanjaro, kitu ambacho
kilimshtua na kuhisi kutapeliwa.
Baada ya hapo, Moshi aliwataarifu
ndugu zake na mara moja msako
mkali dhidi ya tapeli huyo ukaanza.
“Nilipagawa baada ya kujibiwa kuwa
niliyemtumia fedha yuko Kilimanjaro,
jibu hilo lilinichanganya sana,”
alisema Moshi.
Kwa mujibu wa Moshi, alitafuta watu
wa kumsaidia kumkamata mtu huyo
na hatua yao ya kwanza ilikuwa ni
kwenda ofisi za mtandao wa Tigo
zilizopo Mlimani City jijini Dar ili
kujua sehemu halisi alipo tapeli
huyo.
Baada ya kueleza tatizo lao,
mfanyakazi wa kampuni hiyo
aliwaeleza kuwa mtu mwenye namba
hiyo anapatikana eneo la Ubungo
Kibangu, jijini Dar es Salaam.
“Na kweli tulipoenda Kibangu tukiwa
na wenyeji wa huko tulifanikiwa
kumpata kirahisi sana na
kumchukua, kutokana na kibano
alichopewa alisema sio yeye
aliyetapeli bali ni pacha wake,”
alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi
Kinondoni, ACP Camilius Wambura
alikiri kutokea kwa tukio hilo na
kusema mtuhumiwa amekamatwa.
“Tunamchunguza kabla ya kumfikisha
kortini,” alisema.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑