SAKATA KUKAMATWA NA UNGA: RASHID MATUMLA AZUNGUMZA KUHUSU TUHUMA ZINAZOMKABILI MDOGO WAKE

image

Bondia Rashid ‘Snake man’ Matumla
amedai endapo itathibitika mdogo
wake, Mkwanda anajihusisha
kusafirisha dawa za kulevya atakuwa
ameipa fedheha familia yao.
“Mkwanda ameipa fedhea familia
yetu, hii ni aibu kubwa ukizingatia
vitendo hivyo vinakatazwa si
Tanzania tu bali na kwenye nchi
nyingine,” alisema Matumla jana
katika mahojiano na gazeti hili.
Mkwanda ambaye kwa mujibu wa
Rashid alipumzika kucheza ngumi
miaka kadhaa iliyopita kutokana na
kusumbuliwa na  maradhi
alikamatwa wiki iliyopita nchini
Ethiopia akiwa na mchezaji wa
zamani wa Simba, Joseph Kaniki na
leo watapandishwa kizimbani nchini
humo kwa tuhuma hiyo.
“Mimi mwenyewe nashangaa ni lini
amejiingiza kwenye kazi hiyo, hata
wakati anaondoka hakuniaga, mimi
kaka yao na familia hatuelewi
chochote,” alisema Matumla.
Alisema mdogo wake huyo alikuwa
amebadilisha uraia na kuchukua
uraia wa Sweden na kuoa hukohuko
Sweden licha ya kwamba hapa
Tanzania alikuwa amepanga
Mbagala, Dar es Salaam na alikuwa
anakuja na kukaa kwa muda na kisha
kuondoka.
“Ni mwezi sasa umepita sina taarifa
naye na hata wakati anaondoka
hakuniaga, nimesikia kupitia vyombo
vya habari kitendo cha mdogo wangu
kukamatwa kimenisikitisha mno, siyo
siri nimekwazika na ninarudia
kusema hii ni fedheha kwenye
familia yetu,” alisema bingwa huyo
wa zamani wa dunia wa WBU. Rekodi
zinaonyesha kabla ya kupumzika kwa
muda kucheza ngumi, Mkwanda
alishinda mapambano manane (sita
kwa KO) alipigwa mara tatu zote kwa
KO alitoka sare mara moja tangu
2004.
SOURCE: MWANANCHI

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑