Matumla: Napigana ili nisife njaa

image

Dar es Salaam. Licha ya umaarufu
aliowahi kuwa nao bingwa wa
zamani wa dunia wa WBU, Rashid
‘Snake man’ Matumla hali yake
kiuchumi na kiafya imezidi kuwa tete
huku mwenyewe akikiri mambo yake
kumwendea kombo.
Matumla bondia aliyewahi kuiletea
sifa Tanzania miaka ya 1990
aliliambia gazeti hili jana kuwa
amekuwa akipigana kutokana na hali
ngumu ya maisha licha ya maradhi
yanayomkabili kipindi hiki.
“Nadhalilika hivi sasa, maisha yangu
ni magumu mno, nacheza ngumi
kiubishi ili kutafuta fedha ya
kujikimu kila kitu changu hivi sasa
hakiendi vizuri,” alisema bondia
huyo kwa huzuni katika mahojiano
na gazeti hili.
Matumla ambaye alitembelewa na
gazeti hili nyumbani kwake maeneo
ya Keko Mwanga, Dar es Salaam na
kushuhudia maisha yake nje ya
ngumi, alisema hana jinsi zaidi ya
kupigana mapambano ya utangulizi
ili kupata pesa ya kujikimu.
“Kila kitu changu hivi sasa
kinaniendea kombo, nilifanya
biashara ya mahindi huko Tanga
imekufa vivyohivyo na ile ya mbao,
napigana ulingoni nikiwa mgonjwa ili
nipate fedha kwani sina fedha
kabisa,” alisema bondia huyo kwa
masikitiko.
Matumla ambaye anabainisha
kusumbuliwa na mgongo na miguu
anadai hivi sasa anatumia tiba ya
kienyeji baada ya kushindikana
hospitalini na kueleza kuwa alicheza
pambano lake la Agosti 10 mjini
Morogoro na Maneno Oswald
akiamini amepona kumbe ilikuwa
tofauti na maradhi yanayomkabili .
“Napata tabu sana, leo hii
nadhalilika, kila kitu kinaniendea
kombo kweli, nadhalilika ila sina
jinsi,” alisema Matumla kwa
masikitiko.
Bondia huyo aliyewahi kutembelea
gari aina ya Benz enzi zake,
alibainisha kuwa amepigana
mapambano mengi akiwa tayari na
maumivu hayo, lakini alifanya hivyo
ili apate pesa lakini hakuwa na
nguvu za kupigana.
source-mwananchi

posted by kulwa ngatigwa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑