Lowassa ataka viongozi wa kimila kuzuia mmomonyoko wa maadili

image

WAZIRI Mkuu mstaafu na
Mbunge wa Monduli, Edward
Lowassa amesema machifu,
watemi na wakuu wengine wa
kimila wana nafasi kubwa
katika kuzuia mmomonyoko wa
maadili kwenye jamii.
Akizungumza mjini Tabora jana
wakati wa sherehe kuadhimisha
miaka 124 ya shujaa wa
Unyanyembe, Chifu Isike
Mwana Kiyungi, Lowassa
alisema wakuu hao wa kimila
wakitumika wanaweza kusaidia
masuala mbalimbali katika
jamii.
“Hawa machifu wanaweza
kusaidia tatizo hili, Mimi Kule
kwetu Monduli ni Laigwanani
mkuu…kuna wakati hali ya
maambukizi ya Ukimwi yalikuwa
makubwa kwa Wamasai, sasa
nikawaita Malaigwanani
wenzangu nikawaomba
waondoe baadhi ya mila
zinazochangia hali ile,
tukakubaliana na kupita kijiji
kwa kijiji kuelezea na kweli
ikaleta mafanikio maambukizi
yale yakapungua,” alisema.
Aidha alipongeza hatua
iliyofikiwa ya kuenzi
kumbukumbu hiyo na kusema
kizazi cha sasa kina kila sababu
ya kuiga mfano wa Chifu Isike
wa kutetea utu wake.
Maadhimisho hayo yamefanyika
katika kijiji cha Itetemia
ambako ndiko iliko Ikulu ya
chifu huyo wa Unyanyembe,
aliyepigana dhidi ya majeshi
Mjerumani Von Prince (Mwana
Sakaraga) kuanzia mwaka 1889
hadi 1893.
Lowassa aliwataka wakazi wa
Tabora kuwekeza mji wao kitalii
kutokana na historia kubwa ya
mkoa huo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑