SHAHIDI AFARIKI DUNIA MAHAKAMANI AKITOA USHAHIDI

image

Katika hali isiyo ya kawaida, mkazi
wa Kijiji cha Lorwe Kata ya
Nyahongo Shirati, wilayani Rorya,
mkoani Mara, Charles Warito (38),
ambaye ni shahidi wa mlalamikaji
katika Kesi ya kudhuru mwili kwa
kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa
mkono na kusababisha ulemavu
amefariki dunia, wakati akitoa
ushahidi.
Warito alikutwa na umauti huo
akiwa kizimbani katika Mahakama
ya Wilaya ya Tarime mbele ya Jaji
G. Ndika anayesikiliza kesi katika
Wilaya za Tarime na Rorya.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea
jana mchana baada ya
Mwanasheria wa Serikali, Mayega
na Mwendesha Mashitaka wa Polisi
Inspekta George Lutonja walimwita
kuingia Kizimbani tayari kutoa
ushahidi.
Shahidi huyo alianza kutoa
ushahidi wake na alieleza
kushambuliwa kwa kukatwa
mapanga na mtuhumiwa Kichohe
Kichere ambaye ni mkazi wa Kijiji
cha Omoche Kata hiyo ya Nyahongo
Shirati Januari 26, mwaka 2008 na
kutokana na majeraha aliyoyapata
kwa kukatwa mkono na mwili wake
ulianza kupooza na kulemaa
upande wa kulia ambao mkono
ulikatwa
Alipoanza kujibu maswali kutoka
kwa wakili wa mtuhumiwa mara
alianza kulegea na kuishiwa nguvu
na kuanguka kizimbani na kuzimia
hali iliyofanya Mahakama hiyo
Kusitisha Kusikiliza kesi na shahidi
huyo kukimbizwa Hospitali ya
Wilaya kupatiwa matibabu na
alifariki kabla ya kupatiwa
matibabu.
Mtuhumiwa katika kesi hiyo
akiondoka haraka mahakamani
hapo huku ndugu wa marehemu
aliyejitambulisha kwa jina Otieno
Rada alisema: ” Nimesikitishwa na
kifo hiki cha ndugu yangu Charles
Joseph kwani majeraha hayo
aliyoyapata ya kukatwa mkono
na Kichere yalisababisha alemae
mkono na kuanza kupooza na
yamechangia kifo chake.”
Mwili wa marehemu Charles
umehifadhiwa katika Hospitali ya
Wilaya Tarime ukisubili
kuchukuliwa na ndugu zake kutoka
Kijiji cha Lorwe Kata ya Nyahongo
Shirati kwa maziko

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑