TANZANIA YAMKATAA BALOZI MPYA WA UJERUMANI

image

Dar es Salaam. Tanzania
imemkataa Balozi mteule wa
Ujerumani ambaye alitakiwa kuja
kufanya kazi nchini.
Balozi huyo, Margit Hellwig-Boette
alikuwa amemaliza muda wake
nchini Kenya na alitakiwa kuja
kuiwakilisha nchi yake Tanzania.
Balozi Hellwig-Boette alikaririwa na
Gazeti la Standard la Kenya
akieleza kuwa anajipanga kurudi
kwao baada ya kukataliwa na
Serikali ya Tanzania.
Alipoulizwa juu ya suala hilo,
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Sefue alikataa
kuzungumzia suala hilo akisema:
“Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje
ndio wanaoshughulika na hayo
mambo, waulizeni.”
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
cha Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa
Ally alisema wizara yake haijapata
taarifa za kukataliwa kwa balozi
huyo.
“Suala hilo linahusu ofisi ya Rais,
mambo ya uteuzi ni ya Rais. Wizara
ya Mambo ya Nje haina hiyo taarifa
na hata kama ingekuwapo hiyo
taarifa siyo ya `public’.
“Siyo taarifa ya umma kwa maana
kwamba, mchakato wake ni wa siri
na hayo mambo hayana kuuliza
kwa nini. Ukileta jina la mtu
unayetaka aje kuwa balozi
likikataliwa, hakuna kuuliza eti ni
kwa nini.
“Unachofanya ni kuleta jina jingine,
hata Rais hapa akipeleka jina la
mtu kwenye nchi nyingine
lisiporudi, hakuna kuuliza
unachofanya ni kuteua tu jina
jingine,” alisema Mkumbwa.
Alikariri Kifungu cha Nne cha
Azimio la Vienna ambacho
kinaruhusu nchi kukataa balozi wa
nchi nyingine bila ya kutoa sababu.
“Nchi inayopeleka balozi katika
nchi nyingine inatakiwa kutoa jina
mapema kwa nchi nyingine. Hata
hivyo, nchi hiyo ina uwezo wa
kumkubali au kukataa uteuzi,”
kinaelekeza kifungu hicho.
na udaku blog

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑