MWALIMU MKUU ANASWA NA MAGUNIA 6 YA BANGI HUKO MKOANI KAGERA.

image

MWALIMU Mkuu wa Shule ya
Msingi Mukubu, Wilaya ya Ngara
mkoani Kagera, Silidion Kaiza
(43), anashikiliwa na Jeshi la Polisi
kwa tuhuma za kukutwa na bangi
gunia sita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kagera, Philip Kalangi alisema
kuwa tukio hilo lilitokea
Septemba 17, mwaka huu, shuleni
hapo katika kata na kijiji cha
Muganza majira ya saa tano
asubuhi.
Alisema kuwa raia wema walitoa
taarifa kituo cha polisi Rulenge
kwamba kuna mwalimu
anajihusisha na biashara ya kuuza
dawa za kulevya, jambo
walilohofia kuwa huenda
akawaathiri wanafunzi wa shule
hiyo kwani anazihifadhi shuleni.
Kalangi alifafanua kuwa baada ya
polisi kupata taarifa hiyo walifika
shuleni hapo na kumhoji mwalimu
Kaiza, na alikiri kufanya biashara
hiyo kisha akawapeleka katika
moja ya darasa ambalo alikuwa
akitunza bangi hiyo.
Kamanda alisema kuwa baada ya
polisi kukamata bangi hiyo,
waliifikisha kituoni na kwamba
mwalimu huyo anaendelea
kuhojiwa kisha atafikishwa
mahakamani wakati wowote ili
kujibu tuhuma hizo.
Aliwataka wananchi kuendelea
kuwafichua wahalifu
wanaojihusisha na vitendo vya
uuzaji wa dawa za kulevya
ambavyo vimekuwa tishio kwa
taifa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑