BABU AMBILIKILE MWAISAPILA: “NIMEOTESHWA NA MUNGU TANZANIA ITAKUA KIOO CHA AFRIKA NA DUNIA”

image

MCHUNGAJI Ambilikile Mwaisapila
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) amesema Mungu
ameendelea kujifunua kwake na
kumuonyesha kuwa Tanzania itakuwa
kioo cha Afrika na baadaye kioo cha
dunia.
Ametoa kauli hiyo jana asubuhi
(Jumanne, Septemba 24, 2013) mbele
ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati
akizungumza na wakazi wa kijiji cha
Samunge, wilayani Ngorongoro
mkoani Arusha wakati msafara wa
Waziri Mkuu uliposimama nyumbani
kwake ili kumsalimia akiwa njiani
kurejea mjini Arusha.
Mchungaji Mstaafu Mwaisapila
maarufu kama Babu wa Samunge
alisema kuna mambo mengi ambayo
yameandikwa kwenye Biblia lakini
hayakutokea Israeli na sasa
yatafanyika hapa Samunge. “Mungu
ametupenda sana, yanakuja mambo
makubwa na wala hayako mbali.
Kama mimi ni mzee na nitayaona,
kwa hiyo mtarajie kuwa hayako mbali
kutokea,” alisema huku
akishangiliwa.
Alisema katika mafunuo aliyopewa na
Mungu ameonyeshwa kwamba watu
wengi zaidi watafurika kijijini
Samunge kuliko ilivyokuwa hapo
awali. Alitumia fursa hiyo kuishukuru
Serikali kwa misaada iliyotoa wakati
wa ‘kugawa kikombe’ ikiwemo
mahema, maji na ulinzi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑