Nyie ni watu wabaya: Mtoto wa miaka 4 awaambia magaidi

image

Mtoto wa miaka minne ambaye ni
raia wa Uingereza, Elliott Prior
ameonyesha ushujaa wa hali ya juu
baada ya kuweza kuwatolea maneno
makali na ya kugusa magaidi
waliovamia jengo la maduka la
Westgate.
Baada ya maneno hayo, baadhi ya
taarifa zilizochapishwa kwenye
vyombo mbalimbali vya kimataifa,
vinasema magaidi hao waliomba
mtoto huyo awasamehe kwa maelezo
kuwa wao siyo watu wabaya.
Inaelezwa kuwa, kitendo cha mtoto
huyo kilikuwa cha kishujaa kwani
aliweza kuwaeleza magaidi hao
maneno hayo, bila kuogopa silaha
nzito walizokuwa wameshika mkononi
huku baadhi ya watu wakiwa
wameshauuawa.
Mtandao wa Daily Mail unasema
mtoto huyo alimwambia mmoja wa
magaini hao kuwa ‘Nyie ni watu
wabaya sana’.
Mtandao huo unasema mtoto huyo
aliyasema maneno hayo kama njia ya
kumkinga mama yake Amber,
aliyekuwa amepigwa risasi mguuni
pamoja na dada yake Amelie,
mwenye umri wa miaka sita ambaye
walikuwa wote ndani ya duka hilo.
Katika kile kilichotafsiriwa kuwa ni
kuumizwa na maneno hayo, magaidi
hao walimpa Elliott pamoja na dada
yake mifuko miwili miwili ya chokleti
na kuwaomba msamaha.
Taarifa hizo zinasema kuwa, gaidi
huyo alisema “Samahani nisamehe,
sisi siyo watu wabaya”.
Mama huyo anasema kuwa, kabla ya
kukamatwa na magaidi hao, yeye na
watoto wake walikuwa wamejificha
kwenye jokofu la kuhifadhi nyama
lililopo ndani ya duka la Nakumatt
kwa zaidi ya saa moja na nusu.
Anasema kuwa, baada ya kukamatwa
na magaidi hayo, walimpiga risasi ya
paja.
Mjomba wa watoto hao aliliambia
gazeti la The Sun la Uingereza kuwa
“Walikuwa na bahati kuweza kutoka
kwenye mikono ya hao magaidi. Hao
magaidi walisema kuwa, kama kuna
mtoto yeyote aliye hai ndani ya
jengo hilo wanaweza kuondoka.
‘Mama yao alisimama na kusema
‘ndio’ , binamu yangu aliweza kupata
ujasiri wa kusimama na kuwaambia
kuwa, nyie ni watu wabaya sana’.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, baada
ya magaidi hao kujua kuwa mama
huyo na watoto wake hawakuwa kati
ya watu waliowalenga, hawakuwaua.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑