Siku ya kujua kusoma na kuandika : Watu milioni 774 duniani ni mbumbumbu

image

Wakati kiwango cha watu wazima
wasiojua kusoma na kuandika
kikiongezeka kwa asilimia nane
kuanzia mwaka 1990, taarifa ya
utafiti mpya inasema bado kuna
watu milioni 774 duniani wasiojua
kusoma wala kuandika.
Shirika la Umoja wa Mataifa
linalohusika na Elimu, Sayansi na
Utamaduni Unesco, lilitoa ripoti
wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Kujua Kusoma na Kuandika Septemba
nane mwaka huu, iliyosema idadi
kubwa ya watu hao mbumbumbu
wanaishi katika mabara ya Afrika na
Asia.
Pia takwimu za ripoti zinaonyesha
kuwa robo tatu ya wale wasiojua
kusoma na kuandika ni wanawake, na
kwamba hali hiyo inaweza
kuongezeka hata wakati wa kufikiwa
tarehe ya mwisho ya malengo ya
Maendeleo ya Milenia ambayo ni
mwaka 2015.
Katika ujumbe wake kuadhimisha
siku hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa
Unesco Irina Bokova alisema kuwa
dunia inapaswa kujikagua upya.
Alisema kuwa dunia ina wajibu wa
kuboresha mifumo yake ya utoaji wa
elimu, kwani bila kufanya hivyo kuna
uwezekano wa kurudi nyuma
kimaendeleo. “ Tunapaswa kumulika
mifumo yetu ya utoaji elimu ili iende
sambamba na mahitaji ya wakati”
anasema.
Wasiojua kusoma na kuandika
Tanzania
Ripoti hiyo ya Unesco imetolewa
katika wakati ambapo kiwango cha
kujua kusoma na kuandika nchini
kikitajwa kuporomoka.Hadi kufikia
mwishoni mwa mwaka 2002 idadi ya
Watanzania wasiojua kusoma na
kundika ilifikia milioni 6.2.
Akizungumza bungeni, Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk
Shukuru Kawambwa alisema kuwa
idadi hiyo ni kwa watu wenye umri
wa miaka 15 na kuendelea, sawa na
asilimia 31.
Aliongeza kusema kuwa kuna
uwezekanano idadi hiyo ikaongezeka
kutokana na mazingira yaliyopo sasa.
Alieleza kuwa watu wasiojua kusoma
na kuandika hawajamalizika, na
kwamba Sensa ya Watu na Makazi ya
mwaka 2012 bado haikuwa imetoa
mchanganuo wa watu wasiojua
kusoma, kuandika na kuhesabu.
“Ili kuimarisha Elimu ya Watu
Wazima, Serikali inatekeleza mambo
mbalimbali, ikiwemo kuboresha
mpango wa awali wa Elimu ya Watu
Wazima kupitia programu ya ‘Ndiyo
Naweza’ yenye lengo la kupunguza
idadi ya wasiojua kusoma na
kuandika nchini’’ anasema na
kuongeza:
“Serikali inatumia uzoefu
uliopatikana katika utekelezaji wa
Mpango wa Uwiano Kati ya Elimu ya
Watu Wazima na Jamii (MUKEJA),
ambapo mpaka mwaka 2012 ulikuwa
na jumla ya wanakisomo 907,771.’’

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑