WANAUME WAMBEA KULIKO HATA WANAWAKE LAKINI KUMBE UMBEA UNAFAIDA KUBWA KWA UPANDE WA AFYA YA BINADAMU !!!!!.

image

mbea huchukiwa,
hutengwa na hata wakati mwingine
hupigwa kwa kuonekana kuwa ni
chanzo cha migogoro na huku
viongozi wa dini wakimwona mtu
wa aina hiyo kuwa ni mtenda
dhambi.
Watu wanaopenda tabia ya umbea
huenda wakawa wamepata mtetezi.
Ripoti iliyotolewa hivi karibuni
kuhusu tabia ya watu kupenda
kutumia muda mwingi kusema
mambo ya watu wengine, inasema
tabia ya umbea ina manufaa kiafya.
Ripoti hiyo iliyotolewa na watafiti
kutoka chuo kikuu cha Rhode
Island cha Marekani, inasema kuwa
watu wanaonufaika zaidi za tabia
hiyo ni wale wanaopenda kuongea
mambo mabaya wa watu wengine
kuliko wenzao wanaopenda
kuzungumza kuhusu mambo
mazuri.
Wataalamu hao wamebaini kuwa
iwapo mtu atatumia dakika 20
kuzungumzia mambo mabaya ya
watu wengine, anaweza kuimarisha
afya yake kwa kupunguza msongo
wa mawazo, woga na mashaka kwa
asilimia 96 kwa muda wa masaa
manne mfululizo.
Hata hivyo, wamebainisha kuwa
mtu akitumia muda huo huo
kuzungumza mambo mazuri ya
watu wengine, atapunguza msongo
wa mawazo kwa asilimia 72
ikimaanisha kuwa watu wenye
kuzungumza mambo mabaya ndio
wenye kunufaika zaidi.
Watafiti hao, wakifafanua hali hiyo
wameelezwa kuwa mtu anapoongea
habari nzuri zinazowahusu watu
wengine huuchochea ubongo kutaka
kujiunganisha na mtu
anayezungumzwa, wakati yule
anayezungumza habari mbaya
huwa kinyume chake.
Mtu anayezungumza habari mbaya
anatabia ya kutokuhifadhi
alichokisema, bali huendelea na
mambo yake kama kawaida, wakati
anayezungumza habari nzuri hukaa
nazo moyoni kwa kipindi cha muda
fulani.
Mtaalamu wa Saikolojia kutoka
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
, Lusajo Kajula anasema binadamu
wote huongea kuhusu watu
wengine, lakini umbea ni zaidi ya
maongezi.
Lusajo anasema asili ya
mwanadamu ni kuzungumza
japokuwa wakati mwingine
hujikuta akiishia kutoa mifano
halisi ya maisha ya watu wengine
na hivyo kuingia katika mgogoro
wakati mtu aliyesemwa anaposikia.
“Umbea ni kawaida na hauzuiliki,
tatizo ni yaliyomo ndani ya umbea
ambayo mara nyingi hutegemea na
mawazo mtu aliyonayo. Kama ana
mawazo hasi, ataongea mambo
mabaya,” anasema Kajula.
Hata hivyo, Kajula anapingana na
dhana iliyopo miongoni mwa watu
kuwa mwanamke ndiyo anayependa
zaidi tabia ya kuzungumza mambo
ya watu wengine kuliko
mwanaume.
“Kuna tafiti nyingi zinazoonyesha
kuwa wanaume ni wambea zaidi
kuliko wanawake, ila wao
hawasutani na pia hawawezi
kujieleza vizuri kama wanawake,”
anasema Kajula na kuongeza kuwa
kwa kawaida tabia ya kuongea
mambo mazuri yanayowahusu watu
wengine hukusudia kukuza
heshima ya mtu anaezungumziwa.
Mwanasaikolojia na mwandishi wa
kitabu kiitwacho ‘Nguvu ya Umbea’,
Maria Konnikova anasema hakuna
mtu anaeweza kuukwepa umbea na
kushauri kuwa mtu asihangaike
kutaka kuwazuia wambea kusema
wayatakayo.
Anasema wataalamu mbalimbali wa
masuala ya saikolojia wamebaini
kuwa umbea ni njia muhimu katika
kuleta umoja na mshikamano
katika jamii kwani kwa kufanya
hivyo husaidia kueneza taarifa
ambazo wanajamii wasingeweza
kuzifahamu. “Pia imebainika kuwa
umbea ni zana nzuri ya kuifundisha
jamii mtu gani anafaa kuwa rafiki
na yupi anastahili kuepukwa,”
anasema Konnikova.
Mwanasaikolojia Homer Simpson
wakati fulani aliwahi kusema:
“Kama hatutakiwi kula nyama
kwanini wanyama waliumbwa kwa
nyama? Kama kila mtu anafahamu
kuwa umbea ni mbaya kwa nini
anasema? Jibu ni rahisi; katika
ubongo wetu kuna sehemu
inayopenda umbea.”
Anasema kila mtu ananufaika na
mambo mazuri yanayosemwa juu
yake anapoyasikia. “Wapi
ungependa kufanya kazi, sehemu
ambayo watu wanakusema vibaya
au vizuri?”anahoji Simpson.
Mchungaji wa Kanisa la Free
Pentekosti Tanzania (FPCT) Njia
Panda ya Himo, Kilimanjaro,
Elisante Ngailo, akizungumzia
utafiti huo anasema watu
wanaotumia muda mwingi
kuzungumza mambo mabaya
yanayowahusu watu wengine
husema tu bila kufiria.
“Watu wa aina hii hawaumizi
kichwa kufiri sana, wao husema
mambo walioyasikia au kuyaona,
kisha kuendelea na maisha yao,”
anasema Ngailo.
Anaongeza: “Lakini hawa watafiti
wanataka kutuambia kwamba sasa
tuwaseme sana watu kusudi
tupunguze msongo wa mawazo?
Hili haliwezekani” anasema Ngailo.
Kwa maoni yake si sahihi kwa watu
kuwasema watu wengine vibaya na
kwamba tafiti kama hizi hazijengi
jamii kwa kuwa tabia ya umbea
inapingwa na makundi mbalimbali
ya watu.
Maoni ya watu mbalimbali
Roda Mgimwa mkazi wa Vingunguti
anasema matokeo ya utafiti
uliofanywa kuhusu tabia ya umbea
anakubaliana nao kwasababu watu
wa aina hiyo hawana hofu ya jambo
wanalolizungumza.
“Wakati mwingine unaweza
kumsikia mtu anasema umbea
kuhusu mtu fulani ndani ya
daladala bila kujua iwapo yule
anayesemwa ana ndugu yake hapo
au la. Kwa namna hii watu hawa
hawawezi kusumbuliwa na msongo
wa mawazo,” anasema Roda.
KAMA hujui, wanaume ni wambea
zai

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑