DAKTARI FEKI ALIYENASWA MUHIMBILI NI FUNDI UMEME!

image

SIRI imefichuka! Kumbe yule Dokta
Dismas John Macha aliyenaswa kwa
tuhuma za kujifanya daktari katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar,
Jumanne wiki hii, ni fundi wa
umeme wa nyumbani, Risasi
Jumamosi linaianika.
Akizungumza na mwandishi wetu
Jumatano wiki hii, mmoja wa maafisa
wa ngazi ya juu wa Jeshi la Polisi
ambaye hakutaka jina lake liandikwe
kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo,
alisema kwa mujibu wa uchunguzi
wao, ilibainika kwamba dokta huyo
feki ni fundi umeme wa siku nyingi.
Afisa huyo alisema kuwa hadi sasa
uchunguzi zaidi juu ya Macha
unaendelea ili kujua mambo
mengine yaliyojificha.
Hata hivyo, hakuweka wazi ni hatua
gani ambayo anaweza kuchukuliwa
na kusisitiza kuwa lile ni kosa kubwa
kwani linahusisha afya na maisha ya
watu.
“Baadhi ya mambo ambayo
tumeyabaini kuhusu huyu jamaa, ni
kuwa kumbe ni fundi umeme wa
nyumbani na alichokuwa akifanya
Muhimbili ni kutaka kujipatia fedha
kwa mkato japo tunaendelea
kupeleleza kujua ni wapi alipata
vifaa vya udaktari,” alisema na
kuongeza:
“Tuhuma kama hii ni nzito,
inahusisha afya na maisha ya watu
kwa jumla, taratibu zinaendelea
kujua mengi sana juu ya huyu
bwana.”
Macha ambaye anadaiwa kutafutwa
na uongozi wa Muhimbili kwa muda
mrefu, alikamatwa na kufikishwa
kwenye kituo cha usalama cha
Muhimbili (Muhas) kwa mahojiano
zaidi ambapo habari zilidai alisema
yeye ni daktari wa Mwananyamala
ambaye alifika hapo kwa ajili ya
kuangalia wagonjwa wake wa nje.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑