MFUNGWA ANASWA AKIJIUZA

image

BAADA Mei mwaka huu kuhukumiwa
kifungo cha miezi sita gerezani kwa
kosa la kufanya ukahaba, mkazi wa
jijini Dar, Blandina Barton
amekamatwa tena kwa kosa hilohilo
ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya
kumaliza kifungo chake, Risasi
Jumamosi linakupa mkasa mzima.
Habari za uhakika zilizopatikana
katika Mahakama ya Jiji, Dar es
Salaam zinasema kwamba mfungwa
huyo alitumikia kifungo chake katika
Gereza la Segerea jijini Dar na
alipobakiza miezi michache kumaliza
alionewa huruma na bibi jela na
kutakiwa kumalizia kifungo hicho
uraiani.
Inadaiwa kuwa kabla ya kuachiwa,
bibi jela alimsihi Blandina
kuhakikisha harudii kosa
lililompeleka gerezani pindi
atakapokuwa akimalizia kifungo chake
nje ya gereza.
Blandina akamhakikishia bibi huyo
kwamba atakuwa mtu safi kwani
amejifunza vya kutosha.
Katika hali ya kushangaza, Jumatano
iliyopita Blandina alipandishwa tena
katika Mahakama ya Jiji iliyopo
Barabara ya Sokoine jijini Dar akiwa
amerudia kosa lililompeleka Segerea
miezi michache iliyopita.
Imeelezwa mahakamani hapo
kwamba, Septemba 24, mwaka huu
Blandina na wenzake wanne
walinaswa Buguruni usiku wakiwa
katika mawindo ya ukahaba.
Bahati mbaya kwa Blandina
alipofikishwa mahakamani hapo
alikutana na hakimu yuleyule
aliyemhukumu kifungo cha miezi sita
kwa kosa la ukahaba.
Hakimu huyo, Timothy Lyon alipigwa
na butwaa baada ya kumuona
Blandina akiwa amesimama mbele
yake.
Mtuhumiwa huyo aliyekuwa na
wenzake, Husna Amos, Monica Denis,
Esther Chizai na Angela Emmanuel
wote kwa pamoja walisomewa
mashtaka yao na kukana.
Hakimu Lyon aliwaambia
watuhumiwa hao kwamba dhamana
iko wazi na kuwataka kila mmoja
kuwa na wadhamini wawili na
shilingi laki mbili.
Sharti hilo lilionekana kuwa gumu
kwa watuhumiwa wote, hivyo
walipandishwa karandinga na
kupelekwa Gereza la Segerea mpaka
Oktoba 15, mwaka huu kesi yao
itakapotajwa tena mahakamani
hapo.
Mei mwaka huu gazeti dada na hili
la Ijumaa liliandika habari za kifungo
cha Blandina mara baada ya
kuhukumiwa kwenda jela huku
ikidaiwa kwamba msichana huyo ni
mchumba wa mtu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑