Serikali yayafungia Magazeti ya Mwananchi na Mtanzania

image

Serikali imeyafungia kutochapishwa
Magazeti ya MWANANCHI na
MTANZANIA kuanzia 27
Septemba,2013 kutokana na
mwenendo wa magazeti hayo
kuandika habari na makala za
uchochezi na uhasama kwa nia ya
kusababisha wananchi wakose imani
kwa vyombo vya dola hivyo
kuhatarisha amani na mshikamano
ulipo nchini.
Gazeti la MWANANCHI limefungiwa
kutochapishwa kwa siku kumi na nne
(14) kuanzia 27
Septemba,2013.Adhabu hii
imetangazwa kwa Tangazo la Serikali
(Government Notice )Namba 333 la
tarehe 27 septemba,2013.
Gazeti la MWANANCHI limepewa
adhabu hiyo kutokana na hivi
karibuni kuchapisha habari zenye
mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu
wa amani,mfano tarehe 17 Julai,2013
katika toleo Namba 4774 ilichapisha
habari isemayo “MISHAHARA MIPYA
SERIKALINI 2013” kwa kuchapisha
waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya
vyombo vya habari waraka huo
ulikuwa wa Siri haukupaswa
kuchapishwa Magazetini.
Aidha, katika toleo la
Jumamosi,tarehe 17 Agosti,2013
lilichapisha habari yenye kichwa
kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI
YA ULINZI MKALI” habari hiyo
ilikolezwa na picha ya mbwa mkali
mwenye hasira.Habari na picha hiyo
ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi
lilipeleka Mbwa katika maeneo ya
ibada ya waumini wa dini ya
kiislam.Jambo ambalo halikuwa la
ukweli.
Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo
halikupeleka mbwa katika maeneo ya
Misikiti.Serikali na jeshi la Polisi
linaheshimu na kuzingatia maadili
ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi
lake haliwezi kupitisha au kuingiza
mbwa katika maeneo ya ibada.
Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha
habari iliyokolezwa na picha ya
mbwa ni uchochezi wa
kulichonganisha Jeshi la Polisi na
waumini wa dini ya kiislam mbwa ni
najisi hapaswi kuingia katika maeneo
ya ibada.
Gazeti la MTANZANIA limefungiwa
kutochapishwa kwa siku tisini(90)
kuanzia tarehe 27 Septemba,2013
kwa kuchapisha habari zenye
uchochezi.Gazeti hili limeonywa
mara nyingi lirekebishe mtindo wake
wa uandishi wa kichochezi na
lizingatie maadili na Sheria na
Kanuni za fani ya Habari.
Pamoja na kuonywa gazeti hili
halikuonyesha kuzingatia maelekezo
ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika
toleo na 7262 la 20 Machi,2013
liliandika habari yenye kichwa
kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe
12 Juni,2013,toleo Namba 7344
lilichapisha makala isemayo
“MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.
Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18
Septemba,2013 katika toleo Namba
73414 ukurasa wa mbele lilichapisha
Kichwa cha habari kisemacho
“SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa
hiyo ilikolezwa na picha zilizo
unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa
kutumia kompyuta kutapakaza rangi
nyekundu mithili ya damu nyingi
kumwagika .Katika habari hiyo gazeti
hilo limedai bila uthibitisho kuwa
Jeshi la Polisi linahusika na wahanga
waliomizwa na watu wasiojulikana
kwa kumwagiwa tindikali na
waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.
Vile vile gazeti hilo limeishtumu
serikali kuwa goigoi katika
kushughulikia matukio yenye sura ya
kigaidi.
Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya
kichochezi ina lengo la kuwafanya
wananchi wavichukie vyombo vya
ulinzi na usalama wavione kuwa
haviwasaidii.
Kutokana na makosa yalitajwa hapo
juu serikali imelifungia gazeti la
Mtanzania kutochapishwa kwa muda
wa siku tisini(90) kwa Tangazo la
Serikali Namba 332(Government
Notice No.332) la tarehe 27
septemba,2013,.
Serikali inawataka wamiliki,wahariri
na wanahabari kwa ujumla kuwa
makini,kuzingatia weledi,miiko na
madili yataaluma uandishi wa
habari.
Serikali inawataka wamiliki na hasa
wahariri kuhakisha kuwa habari
wanazoziandika na vipindi
wanavyoviandaa vinazingatia
taaluma,kuweka mbele maslahi ya
taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa
hali ya juu.
Serikali inavionya vyombo vya habari
vinavyoutumia uhuru wa habari bila
wajibu kuwa haitasita kuvichukulia
hatua kali ikiwemo ya
kuvifungia .Serikali haitakubali kuona
vyombo vya habari kuwa chanzo cha
uvunjifu wa amani nchini.
Imetolewa na
MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA,
UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑