BABU SEYA , PAPII KOCHA .. . KAZI IMEKWISHA

image

MABERE Nyaucho Marando,
wakili wa mwanamuziki maarufu
nchini, Nguza Viking ‘ Babu
Seya’ na mwanaye Johnson
Nguza ‘ Papii Kocha’ amesema
amemaliza kazi ya kuwatetea
wafungwa hao waliohukumiwa
kifungo cha maisha jela baada
ya kukutwa na hatia ya
kuwanajisi watoto 12 waliokuwa
wakisoma Shule ya Msingi
Mashujaa, Sinza jijini Dar es
Salaam .
Akizungumza na gazeti hili juzi,
Marando alisema kazi
aliyokusudia kuifanya
ameimaliza, sasa anasubiri
majaji waliosikiliza alichokisema
ili watoe uamuzi wa mwisho
lakini pia anamtegemea
Mungu.
“Mimi kazi nimemaliza sasa
nawasubiri hao wakubwa
(majaji) ili wapime
nilichowaambia kwa mujibu wa
sheria na kisha watoe uamuzi,
lakini pia namtegemea Mungu, ”
alisema Marando .
Alisema ameiomba Mahakama
ya Rufaa Tanzania ifanye
marejeo kuhusu hukumu
iliyoitoa na ifute ushahidi
uliowatia hatiani wateja wake
hao na adhabu ya kifungo cha
maisha jela wanayoitumikia kwa
sasa.
Alipoulizwa alitumia muda gani
kuwasilisha hoja zake hizo,
Marando alisema takriban
dakika 120 mbele ya jopo la
majaji watatu wa mahakama
hiyo, wakiongozwa na Jaji
Nathalia Kimaro akisaidiana na
Jaji Mbarouk Mbarouk na Jaji
Salum Massati .
Akiwa mahakamani hapo ,
Marando alidai kuwa mahakama
iliteleza katika kutoa uamuzi
uliowatia hatiani na kuwafunga
maisha wateja wake na kwamba
kuteleza huko kunaonekana
waziwazi.
Alifafanua kuwa wakati
wakifanya majumuisho ya kesi
hiyo, mahakama ilijiridhisha
kwamba kulikuwa na makosa
katika kupokea ushahidi wa
watoto wanaodaiwa kufanyiwa
vitendo hivyo .
Alidai kuwa ushahidi wa watoto
hao ulichukuliwa bila ya
kufuata taratibu za uchukuaji
wa ushahidi wa watoto.
Alieleza kuwa mtoto anayesoma
shule kuanzia ya msingi
anapotoa ushahidi licha ya
tahadhari, ana uwezo wa
kutambua zuri na baya na
kwamba lazima ushahidi wake
uwekwe kwenye kumbukumbu
ya maandishi na kwamba
usipoonekana ushahidi wote ni
batili na unaondolewa.
Katika shauri hilo upande wa
Mkurugenzi wa Mashtaka
uliwakilishwa na Mawakili
Jackson Mlaki , Angaza
Mwaipopo, Emakulata Banzi,
Joseph Pande na Apimack
Mbarouk ambao waliyapinga
maombi hayo kuhusu marejeo
kwa madai kuwa yamepelekwa
mahakamani bila usahihi .
Mahakama hiyo imesema itatoa
uamuzi wake siku
itakayotangaza.
Babu Seya na Papii Kocha wako
jela kwa makosa 10 ya kubaka
watoto wa kike wenye umri kati
ya miaka sita na minane na
mengine 11 ya kulawiti watoto
wa kike wenye umri kama huo.
Walidaiwa kutenda makosa hayo
kati ya Aprili na Oktoba 2003
eneo la Sinza Kwaremy jijini
Dar es Salaam . Katika kesi hiyo,
Mwalimu wa Shule ya Msingi
Mashujaa, Sigirinda Ligomboka
ambaye alishitakiwa kwa makosa
mawili ya kumsaidia Babu Seya
kutenda makosa hayo kwa
kuwaruhusu baadhi ya
wanafunzi hao kutoka
madarasani, aliachiwa huru na
Mahakama ya Kisutu
credit GPL

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑