BABU WA MIAKA 82 AUAWA KWA KUVUNJWA SHINGO NA MPWA WAKE KATIKA KIJIJI CHA PERA – CHALINZE PWANI

image
Marehemu mzee Halfan
Mohammed Mtonga enzi za uhai
wake

Stori ya kifo cha mzee Halfan
Mohammed Mtonga (82) mkazi wa
Kijiji cha Pera, Chalinze, Wilaya ya
Bagamoyo mkoani hapa
kinachodaiwa kutokana na
kuvunjwa shingo,
inasikitisha.Tukio hilo lilitokea
Julai 3, mwaka huu nyumbani
kwake baada ya kuzidiwa, hali yake
ilipobadilika siku kadhaa tangu
aliporuhusiwa hospitalini.

image
Marehemu mzee Halfan
Mohammed Mtonga (82) mkazi wa
Kijiji cha Pela, Chalinze, Wilaya ya
Bagamoyo mkoani Pwani
akisindikizwa katika safari yake ya
mwisho.

Akisimulia tukio zima kwa
majonzi, mjane wa marehemu
Aisha Amir (75) alisema, ameumia
sana kumpoteza mume wake
kipenzi ambaye anadai kukatishwa
uhai na mpwa wake aliyemtaja kwa
jina moja la Sabata
aliyemshambulia na kumvunja
shingo.
“Siku ya tukio tulikuwa tumelala
mimi na mume wangu, ghafla
tukaona mwanga wa tochi,
tulipofuatilia tukagundua ni
Sabata, nilipomwambia anataka
nini, akatishia kuniua. Alisema
nikae kimya.
“Alimwamrisha marehemu aamke
ili ampe chipsi na soda alizomletea
lakini alikataa kutokana na hali
yake kiafya kuwa mbaya. Alipoona
amekataa, alimsukuma chini kwa
nguvu, mzee akaanza kulia
akilalamikia maumivu makali ya
shingo. Tukiwa tumeduwaa, Sabata
alianza kumwagia haja ndogo
usoni,” alisema Bi. Aisha akimwaga
machozi.
Alisema baada ya tukio hilo,
majirani waliitana kisha
kumkimbiza hospitalini kwa
matibabu ambapo uchunguzi
ulionyesha kuwa alivunjika shingo.
“Hata hivyo alifanyiwa matibabu
na kuruhusiwa, akaonekana kuwa
na hali ya kuridhisha kabisa, hadi
hali yake ilipobadilika nyumbani
na kufariki,” alisema Bi. Aisha.
Naye mtoto wa marehemu, Seleman
Halfan alisema muda mfupi kabla
ya baba yake kufariki, alikuwa
akilalamika kuuawa na mpwa wake
Sabata.
“Mzee wangu amekufa kifo kibaya
sana, sijui ni kwa nini huyo Sabata
alifikia hatua hiyo. Kila wakati
alikuwa anasema; Sabata unaniua,
Sabata unaniua! Yaani ametuacha
na maswali mengi sana. Lakini
tunaamini sheria itafuata mkondo
wake,” alisema Seleman.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na
kufikishwa katika Kituo cha Polisi
Chalinze kisha kupelekwa
mahabusu katika Gereza la Mifugo
la Ubena, Chalinze mkoani hapa
akisubiri hatua zaidi za kisheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,
SACP Nesphory Matei alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo
aliwataka wananchi kutoa taarifa
kwa vyombo vya dola dhidi ya watu
wasio wema kwenye jamii.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑