UWOYA BANA ! AFANYA FUJO KUBWA NYUMBANI KWA MUME WA MTU

image

NYOTA wa sinema za Kibongo, Irene
Pancras
Uwoya amesababisha tena ! Safari hii
amekinukisha
nyumbani kwa mwanaume aliyewahi
kuwa mpenzi
wake ( jina tunalo) kufuatia jamaa
huyo kufunga
ndoa na mwanamke mwingine na
kumfanya Uwoya
kuendelea kuwa ‘ nyumba ndogo ’ .
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu
hiyo ilichukua
nafasi juzikati, nyumbani kwa
mwanaume huyo,
Sinza- Mori jijini Dar es Salaam.
Nyota wa sinema za Kibongo, Irene
Pancras Uwoya
MCHEZO ULIVYOKUWA
Chanzo kilidai kwamba , siku ya
tukio , Uwoya akiwa
na baadhi ya mastaa wenzake
( hawakutajwa)
kwenye kambi ya maandalizi ya
kurekodi filamu
mjini Bagamoyo , Pwani, alipokea
simu
iliyomnyetishia kuwa , mpenzi wake
huyo amefunga
ndoa na mwanamke mwingine jijini
Mwanza , kwa
hiyo yeye aliye tu !
UWOYA ACHANGANYIKIWA
“Uwoya alipopata salamu hizo kwa
njia ya simu
alichanganyikiwa ! Alianza kusema
maneno ya
kumshutumu waziwazi huku
akiangua kilio . Mbaya
zaidi aliyemjulisha ishu hiyo alisema
ndoa hiyo
ilishafungwa na si kwamba ipo
kwenye maandalizi .
“Akasema anaondoka kambini
kumfuata jamaa yake
na kwamba atamtambua kwani nia
yake ilikuwa
kwenda nyumbani kwake kumfanyia
fujo na huyo
mke mpya , ” kilisema chanzo hicho
cha uhakika .
Nyumba anayodaiwa kufanya fujo
AANZIA DUKANI
Chanzo kilizidi kudai kwamba, licha
ya wasanii
wenzake kumsihi asichukue hatua
hiyo anaweza
kuishia polisi , Uwoya hakukubali,
aliondoka kwa
hasira na breki yake ya kwanza
ilikuwa kwenye
duka kubwa la jamaa huyo lililopo
Mikocheni , Dar
ambapo alifanya fujo.
“Kule alipogundua huyo mwanaume
wake hayupo
ndiyo akaondoka hadi nyumbani
kwake, Sinza
ambako aliendeleza fujo zake kwa
kutukana na
kutishia mambo mengi, ” chanzo
kilisema .
HASIRA PEMBENI
Kwa mujibu wa chanzo, ni dhahiri
kuwa , Uwoya
aliondoka eneo hilo baada ya kuanza
‘ kujaza
nzi ’ ( watu kuwa wengi ) ambapo
aliondoka
mdogomdogo na kama hana hasira
utadhani si yeye
aliyekuwa akichafua hali ya hewa .
MATEGEMEO YAKE
Habari za ndani ziliendelea kudai
kuwa , Irene
alishikwa na hasira za jamaa huyo
kuoa kwa vile
alikuwa akiamini zali hilo lingetua
kwake baada ya
ndoa yake na msakata kabumbu wa
Rwanda,
Hamad Ndikumana ‘ Katauti’ kwenda
halijojo!
“Uwoya alitegemea angeolewa yeye,
sasa kusikia
jamaa kaoa mwanamke mwingine
tena kwa siri,
ilimfanya aishiwe nguvu ,” kilisema
chanzo.
ALICHOAMINI
Habari zinazidi kudai kwamba,
alichoamini Uwoya ni
kwamba kitendo cha mwanaume
huyo kuoa
kingemfanya yeye aendelee kuwa ‘
nyumba ndogo ’
jambo ambalo hakupenda kulisikia
hata kidogo .
UWOYA HUYU HAPA
Baada ya gazeti hili kunyetishiwa
filamu nzima,
lilimsaka staa huyo na kubahatika
kukutana naye
maeneo ya Sinza Palestina jijini Dar
ambapo alikiri
kutokea kwa tukio hilo na kusema
kwamba,
alishaachana na mwanaume huyo.
“Ilitokea, lakini nilishaachana naye .
Unajua ishu si
kwamba angenioa mimi , ila kitendo
alichokifanya
hakikuwa cha uungwana , ” alisema
Uwoya .
AMWANGA CHOZI
Katika hali isiyotarajiwa , msanii huyo
alianza
kumwaga chozi bila kusema sababu
hata pale
alipoulizwa kama chozi hilo lilitokana
na kukumbuka
tukio la jamaa yake kufunga ndoa
kwa siri au la!
Uwoya: “We niache tu , nina mambo
mengi sana
yanayoniliza mimi .”
Kwa upande wake mwanaume huyo
alipopatikana
kwa njia ya simu na kueleza ishu
nzima alijibu kwa
kifupi: “Haiwahusu .” Kisha akakata
simu.
HISTORIA
Uwoya na Ndikumana walifunga
ndoa Julai 11, 2009
kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph,
Jimbo Kuu la
Dar es Salaam. Mei 8, 2011
walijaliwa kupata mtoto
wa kiume aitwaye Krish .
Hata hivyo , Novemba 16, 2011
kwenye gazeti hili
kuliandikwa habari yenye kichwa;
NDOA YA UWOYA YAVUNJIKA.
Ndoa hiyo iliparaganyika baada ya
Uwoya kudaiwa
kumkataa mwanaume huyo na
mpaka sasa
haijasimama tena huku mwanaume
akiwa kwao ,
Rwanda.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Up ↑